Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Yohana Knox

  Hamilton na Wishart, pamoja na mstari mrefu wa wanafunzi wapole, wakatoa maisha yao kwa kigingi. Lakini kutoka kwenye tuta la kuni moto wa Wishart kukatokea mtu ambaye ndimi za moto hazikumunyamazisha, mtu ambaye, chini ya uongozi wa Mungu ilipashwa kupinga onyo la mauti kwa kanisa la Papa katika inchi ya Scotland.TSHM 116.3

  John Knox akatupia mbali maagizo ya asili ya kanisa na akajilisha kwa ukweli wa Neno la Mungu. Mafundisho ya Wishart yakathibitisha kusudi lake la kuachana na Roma na kujiunga mwenyewe na Watengenezaji walioteswa.TSHM 116.4

  Aliposhurutishwa na wenzake kufanya kazi ya kuhubiri, akarudi anapotetemeka mbele ya madaraka kama hayo. Ilikuwa tu baada ya siku za vita kali pamoja naye ndipo akakubali. Lakini alipokubali, akaendelea mbele na uhodari wa kutisha. Ujasiri huu wa mtengenezaji haukuogopa mtu. Alipoletwa uso kwa uso na malkia wa Scotland, Yohana Knox hakukubali kushindwa kwa sababu ya kubembelezwa; hakutetemeka juu ya vitisho. Kwamba Malkia akatangaza kwamba alifundisha watu kukubali dini iliyokatazwa na serekali, na kwa hivyo alivunja pia amri ya Mungu inayolazimisha watu kutii watawala wao. Knox akajibu kwa ujasiri: “Kama watoto wa Izraeli wote walikubali dini ya Farao ambao walikuwa watu wake, nakuuliza, Bibilia, ni dini ya namna gani ingaliweza kuwa katika dunia? Ao kama watu wote katika siku za mitume, wangalikuwa wa dini ya wafalme wa Roma, ni dini ya namna gani ingalikuwa mbele ya uso wa dunia?”TSHM 116.5

  Akasema Marie: “Mnatafsiri Maandiko kwa namna ingine, na (Wakatoliki wa Roma) wanatafsiri kwa namna ingine; nitamwamini nani, na ni nani atakuwa mwamzi?”TSHM 117.1

  “Utamwamini Mungu, ile inasemwa wazi katika Neno lake,” akajibu Mtengenezaji. ... Neno la Mungu linakuwa wazi ndani yake lenyewe; na kama kukionekana giza lolote katika mahali fulani, Roho Mtakatifu, asiyekuwa na mabishano kati yake mwenyewe, hueleza namna moja wazi zaidi mahali pengine.”TSHM 117.2

  Kwa moyo usio na hofu Mtengenezaji shujaa, kwa ajili ya maisha yake, akaendelea na kusudi lake, hata Scotland ikapata uhuru kutoka kwa kanisa la Papa.TSHM 117.3

  Kuimarishwa kwa dini ya Kiprotestanti kama dini ya taifa katika Uingereza kulituliza mateso lakini bila kuikomesha kabisa. Mengi katika maagizo ya Roma yaliendelea. Mamlaka ya Papa ilikataliwa, lakini mahali tu ambapo mfalme alipewa kiti kama kichwa cha kanisa. Katika ibada watu walikuwa wakingali mbali na utakatifu wa injili. Uhuru wa dini ulikuwa haujafahamika. Ijapo matatizo ya kutisha ambayo Roma ilitumia ilipata kimbilio lakini kwa shida na wakuu wa Kiprotestanti, kwani haki ya kila mtu kuabudu Mungu kufuata zamiri yake mwenyewe haikukubaliwa. Wakaidi walipata mateso kwa mamia ya miaka.TSHM 117.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents