Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Moyo wa Wesley “Kwa Jinsi Isiyo ya Kawaida Watiwa Joto”

    Kwa kurudi kwake Uingereza, Wesley akafikia kwa kufahamu wazi wazi imani ya Biblia chini ya mafundisho ya mtu wa Moravia. Kwa mkutano wa chama cha Wamoravian katika Londoni maneno yakasomwa kutoka kwa Luther. Namna Wesley alipokuwa akisikiliza, imani ikawashwa ndani ya roho yake. “Nilisikia moyo wangu kutiwa joto ngeni,” akasema. “Nilisikia kwamba nilimtumaini Kristo, Kristo pekee, kwa ajili ya wokovu: na tumaini likatolewa kwangu, kwamba aliondoa mbali zambi zangu, hata zangu, na aliniokoa kutoka kwa sheria ya zambi na mauti.’‘ TSHM 119.3

    Sasa aliona kwamba neema aliyojitahidi kupata kwa njia ya maombi na kufunga na kujinyima ilikuwa zawadi, “bila mali na bila bei.” Roho yake yote ikawaka na mapenzi ya kutangaza po pote injili utukufu ya neema huru ya Mungu. “Nikatazama juu ya ulimwengu wote kama mtaa wangu,” akasema; “po pote ninapokuwa, ninazania kwamba, nina haki, na wajibu wangu wa lazima, kutangaza kwa wote wale wanaotamani kusikia, habari za furaha za wokovu.”TSHM 119.4

    Akaendelea na maisha yake halisi na ya kujinyima, si sasa kama msingi, bali matokeo ya imani; si shina, bali tunda la utakatifu. Neema ya Mungu katika Kristo itaonekana katika utii. Maisha ya Wesley ilitolewa kuwa wakfu kwa kuhubiri kweli kubwa aliyoyakubali--kuhesabiwa haki kwa njia ya imani katika damu ya kafara ya Kristo, na uwezo mpya wa Roho Mtakatifu kwa moyo, kuendelea kuleta matunda katika maisha yanayofanana kwa mfano wa Kristo.TSHM 120.1

    Whitefield na Wesleys wawili waliitwa kwa wakati ule “Methodistes” na wanafunzi wenzao wabaya -jina ambalo kwa wakati huu linazaniwa kuwa la heshima. Roho Mtakatifu aliwalazimisha kuhubiri Kristo na Yeye aliyesulubiwa. Maelfu waliogeuka kwa kweli. Ilikuwa ni lazima kwamba kondoo hizi zilindwe kutoka mbwa mwitu wenye wazimu. Wesley hakuwa na wazo la kuanzisha dini lingine, lakini aliwatengeneza chini ya kile kilichoitwa mwunganisho wa Methodiste.TSHM 120.2

    Ulikuwa ushindani wa siri na taabu ya uinzani ambayo wahubiri hawa walipambana nayo kwa kuanzisha kanisa--kwani kweli ilikuwa na mwingilio mahali milango labda ingedumu kuendelea yenye kufungwa. Wakuu wengine wa dini wakaamka kwa mshangao wa tabia yao na wakawa wahubiri wa juhudi katika mitaa yao wenyewe.TSHM 120.3

    Kwa wakati wa Wesley, watu wa vipawa mbalimbali hawakulinganisha kila sehemu ya mafundisho ya dini. Tofauti kati ya Whitefield na Wesleys wawili ilitisha wakati moja kuleta fitina, lakini kwa namna walijifunza upole katika chuo cha Kristo, uvumilivu na upendo vikawapatanisha. Hawakuwa na wakati wa kubishana, wakati ambao makosa na maovu yalijaa pote.TSHM 120.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents