Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    13 / KATIKA UHOLANDI NA SCANDANAVIA

    Katika Uholandi ukali wa Papa ukaleta haraka upinzani. Miaka mia saba kabla ya Luther, askofu wa Roma kwa uhodari akashitakiwa na maaskofu wawili, waliotumwa kuwa mabalozi huko Roma, wakajifunza tabia ya kweli ya “jambo takatifu la askofu”; “Unakaa mwenyewe ndani ya hekalu la Mungu; baada ya mchungaji unakuwa mbwa mwitu kwa kondoo, ... lakini ulipashwa kuwa mtumishi wa watumishi, kama upendavyo kujiita mwenyewe, unatumaini kuwa bwana wa mabwana. ... Unaleta haya kwa amri za Mungu.”TSHM 110.1

    Wengine wakatokea katika karne zote kukariri kukataa huku. Biblia ya Wavaudois ilitafsiriwa katika lugha ya Kijeremani. Wakatangaza “kwamba hapo kulikuwa faida ndani yake; hakuna mizaha wala uongo, wala mambo ya michezo, wala udanganyifu, bali maneno ya kweli.” Ndivyo waliandika rafiki za imani ya zamani tangu karne ya kumi na mbili.TSHM 110.2

    Sasa wakati wa mateso ya kanisa la Roma ikaanza; lakini waaminifu wakaendelea kuongezeka, kutangaza kwamba Biblia ni mamlaka pekee ya haki katika dini na kwamba “hakuna mtu anayepashwa kushurutishwa kuamini, bali angepashwa kusadikishwa kwa njia ya mahubiri.”TSHM 110.3

    Mafundisho ya Luther yakapata katika Uholandi watu wa juhudi na waaminifu kwa kuhubiri injili. Menno Simons, mtu wa elimu mkatoliki na aliyetakaswa kwa upadri, alikuwa mjinga kabisa wa Biblia na hakuisoma kwa ajili ya hofu ya upinzani wa ibada ya dini. Kwa ondoleo la zambi akajitahidi kunyamazisha sauti ya zamiri, lakini bila manufaa. Baada ya wakati akaongozwa kujifunza Agano Jipya; hili pamoja na maandiko ya Luther ikamletea kukubali imani ya matengenezo. Kwa mda kitambo akashuhudia mtu aliyeuawa kwa sababu alibatizwa mara ya pili. Jambo hili likamwongoza kujifunza Biblia kwa ajili ya ubatizo wa watoto wadogo. Aliona kwamba toba na imani vinahitajiwa kuwa sababu ya ubatizo.TSHM 110.4

    Menno akatoka kwa kanisa la Roma na akajitoa wakfu kwa kufundisha maneno ya ukweli aliyokubali. Katika Ujeremani na Uholandi kundi la washupavu likatokea, kuharibu kanuni na adabu, na kuendelea kufanya maasi. Menno kwa nguvu zake zote akapinga mafundisho ya uongo na mashauri ya ushenzi ya washupavu. Kwa miaka makumi mbili na tano akapitia Uhollande na upande wa kaskazini ya Ujeremani, kutumia mvuto mkubwa sana, kufananisha katika maisha yake mwenyewe mafundisho aliyofundisha. Alikuwa mtu wa haki, mpole na mtulivu, mwaminifu na mwenye bidii. Hesabu kubwa ya watu wakageuka sababu ya kazi zake.TSHM 110.5

    Katika Ujeremani Charles V alikomesha Matengenezo, lakini watawala wakasimama kama boma juu ya utawala wa ukaidi wake. Katika Uhollande mamlaka yake ilikuwa kubwa sana. Amri za mateso zikafuatana kwa upesi. Kwa kusoma Biblia, kuisikia ao kuihubiri, kumwomba Mungu kwa siri, kukataa kusujudu mbele ya sanamu ao kuimba Zaburi ilikuwa azabu ya kifo. Maelfu waliangamia chini ya Charles na Philip II.TSHM 111.1

    Kwa wakati moja jamaa lote lilipelekwa mbele ya watu wa hekimu (Inquisiteurs), juu ya kutokwenda kwa misa na kuabudu nyumbani. Kijana wa mwisho katika jamaa akajibu “Tunapiga magoti yetu, na kuomba kwamba Mungu apate kuangaza akili zetu na kusamehe zambi zetu; tunaombea utawala wa mfalme wetu, ili ufalme wake upate kusitawi na maisha yake yawe ya furaha; tunawaombea waamzi wetu, ili Mungu apate kuwalinda.” ‘’Baba na mmojawapo wa watoto wake wakahukumiwa kifo cha (kigingi) mti wa kuchoma upinzani wa ibada ya dini.”TSHM 111.2

    Si wanaume tu lakini wanawake na vijana wanawake wakatumia ujasiri imara. “Bibi waliweza kusimama kwa vigingi vya waume wao, na wakati walipokuwa wakivumilia mchomo wa moto wangenongoneza maneno ya faraja ao kuimba zaburi kuwatia moyo.” “Wasichana wakalazwa ndani ya kaburi zao kana kwamba walikuwa wakiingia katika chumba chao kulala usiku; ao kwenda kwa jukwaa na moto, wakijivika kwa mapambo yao mazuri sana, kana kwamba walikuwa wakienda kwa ndoa yao.”TSHM 111.3

    Mateso yakazidisha hesabu ya washuhuda kwa ajili ya ukweli. Mwaka kwa mwaka mfalme akashurutisha kazi yakeya ukatili, lakini hakufaulu. William wa Orange mwishowe akaleta uhuru wa kuabudu Mungu katika Holandi.TSHM 111.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents