Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  28 / KUSIMAMA MBELE YA HABARI YA MAISHA YETU ZILIZOANDIKWA

  “Nikaangalia hata viti vya enzi vilipowekwa, na mmoja aliye mzee wa siku akaketi: mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi, kiti chake cha enzi kilikuwa ndimi za moto, na magurudumu yake moto unaowaka. Na mto wa moto ukatoka, ukapita mbele yake, elfu ya maelfu wakamutumikia, na elfu kumi mara elfu kumi walisimama mbele yake: hukumu ikawekwa, vitabu vikafunguliwa.” Danieli 7:9,10. R.V.TSHM 232.1

  Ndivyo ilivyoonyeshwa kwa njozi ya Danieli siku kubwa wakati maisha ya watu inapopita katika mkaguo mbele ya Mwamzi wa dunia yote. Mzee wa Siku ni Mungu Baba. Yeye, chemchemi ya viumbe vyote,kisima cha sheria yote, anapaswa kuongoza katika hukumu. Na malaika watakatifu kama wahuduma na washuhuda, wanahuzuria.TSHM 232.2

  “Na tazama, pamoja na mawingu ya mbingu alikuja mmoja aliye mfano wa mwana wa watu, akakaribia huyu Mzee wa Siku, wakamuleta karibu mbele yake. Akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wote, mataifa yote, na lugha zote wamutumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, isiyopita kamwe, na ufalme wake ufalme usioweza kuangamizwa.” Danieli 7:13,14.TSHM 232.3

  Kuja kwa Kristo kunakoelezwa hapa si kuja kwake kwa mara ya pili duniani. Anakuja kwa Mzee wa Siku katika mbingu kupokea ufalme ambao utatolewa kwake wakati wa mwisho wa kazi yake kama mpatanishi. Ni kuja huko, na si kuja kwake kwa mara ya pili dunianini, ile iliyopashwa kufanyika kwa mwisho wa siku 2300 katika mwaka 1844. Kuhani wetu Mkuu anaingia Pahali patakatifu pa patakatifu kushughulika katika kazi yake ya mwisho kwa ajili ya mtu.TSHM 232.4

  Katika huduma ya mfano ila wale ambao zambi zao zilihamishwa kwa Pahali patakatifu walikuwa na sehemu katika Siku ya Upatanisho. Vivyo hivyo katika upatanisho kubwa wa mwisho na hukumu ya uchunguzi kesi zilizoangaliwa ni zile za watu wa Mungu wanaojulikana. Hukumu ya waovu ni kazi iliyotengwa na itafanywa baadaye. “Hukumu inapashwa kuanza katika nyumba ya Mungu.” 1 Petro 4:17.TSHM 232.5

  Vitabu vya ukumbusho katika mbingu vianapaswa kuamua matokeo ya hukumu. Kitabu cha uzima kinakuwa na majina ya wote walioingia daima kwa kazi ya Mungu. Yesu aliambia wanafunzi wake: “Lakini furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa katika mbingu.” Paulo anasema juu ya watumishi wenzake, “Walio na majina yao katika kitabu cha uzima.” Danieli anatangaza kwamba watu wa Mungu watakombolewa, “kila mtu atakayeonekana ameandikwa katika kitabu.” Na mfumbuaji anasema kwamba wale tu watakaoingia Mji wa Mungu ambao majina yao “walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.” Luka 10:20; Wafilipi 4:3; Danieli 12:1; Ufunuo 21:27.TSHM 232.6

  Katika “Kitabu cha ukumbusho” kumeandikwa matendo mema ya “wale wenye kuogopa Bwana, na kufikiri juu ya jina lake.” Kila jaribu lililostahimiliwa, kila uovu uliozuiwa, kila neno la huruma lililoonyeshwa, kila tendo la (kafara), kila huzuni iliyovumiliwa kwa ajili ya Kristo imeandikwa. “Umehesabu kutangatanga kwangu; Utie machozi yangu ndani ya chupa yako; Haya si katika kitabu chako?” Malaki 3:16; Zaburi 56:8.TSHM 233.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents