Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mabishano (Wafuasi wa kanisa la Roma)

    Kwa kuona namna mateso ya kutangaza kazi ya Luther katika Ujeremani haikufanya kitu, Warumi wakakusudiakuwe mabishano na Zwingli. Walikuwa na hakika ya ushindi kwa kuchagua si makali tu pa vita bali waamuzi waliopashwa kuamua kati ya wabishanaji. Na kama wangeweza kupata Zwingli katika uwezo wao, wangefanya angalisho ili asikimbie. Shauri hili, basi, likafichwa kwa uangalifu.TSHM 83.2

    Mabishano yalipaswa kuwa huko Bade. Lakini Baraza la Zurich, kuzania makusudi ya watu wa Papa na walipoonywa juu ya vigingi vya moto vilivyowashwa katika makambi ya wakatoliki kwa ajili ya washahidi wa injili, wakamkataza mchungaji wao kujihatarisha maisha yake. Kwa kwenda Bade, mahali damu ya wafia dini kwa ajili ya ukweli ilikuwa imetiririka, ingeleta kifo kweli. Oecolampadius na Haller wakachaguliwa kuwa wajumbe wa Watengenezaji, wakati Dr. Eck mwenye sifa, akisaidiwa na jeshi la watu wenye elimu sana na wapadri, alikuwa ndiye shujaa wa Roma.TSHM 83.3

    Waandishi wakachaguliwa wote kwa wakatoliki, na wengine wakakatazwa kuandika ao wasipotii wauwawe. Mwanafunzi mmoja, aliyeshiriki katika mabishano akaandika abari kila jioni juu ya mabishano yaliyofanyika mchana ule. Wanafunzi wawili wengine wakaagizwa kutoa kila siku barua za Oecolampadius, kwa Zwingli huko Zurich. Mtengenezaji akajibu, anapotoa shauri. Kwa kuepuka uangalifu wa mlinzi wa milango ya mji, wajumbe hawa walileta vikapo vya bata juu ya vichwa vyao na wakaruhusiwa kupita bila kizuizi.TSHM 83.4

    Zwingli “alitumika zaidi,” akasema Myconius, “kwa mawazo yake, kukesha kwake usiku, na shauri alilopeleka Bade, kuliko angeweza kufanya kwa kubishana mwenyewe katikati ya adui zake.”TSHM 84.1

    Wakatoliki wakafika Bade na mavazi ya hariri ya fahari sana ya mapambo ya vitu vya damani. Wakasafiri na anasa sana, na kukaa kwa meza zilizojaa vyakula vitamu sana na divai nzuri sana. Kukawa tofauti kubwa sana kati yao na Watengenezajiambao chakula chao cha kiasi kikawakalisha kwa mda mfupi tu mezani. Mwenyeji wa Oecolampade, aliyempeleleza chumbani mwake, akamkuta akijifunza kila wakati ao akiomba, na akajulisha kwamba mpinga imani ya dini huyo alikuwa “mtawa sana.”TSHM 84.2

    Katika mkutano, “Eckakapanda na majivuno katika mimbara iliyopambwa vizuri sana, lakini mnyenyekevu Oecompade, aliyevaa mavazi ya kiasi, akalazimishwa kuchukua kiti chake mbele ya mpinzani wake kwa kiti kilichochorwa vibaya sana.” Sauti ya nguvu ya Eck na majivuno mingi hakumtisha. Mtetezi wa imani alikuwa anatazamia mshahara mzuri. Wakati alipokosa mabishano bora, akatumia matukano na hata maapizo ama laana.TSHM 84.3

    Oecolampade, mwenye adabu na mwenye kujihazari, akakataa kushiriki katika mabishano. Ingawa alikuwa mpole na adabu katika mwenendo, akajionyesha mwenyewe kuwa na uwezo na imara. Mtengenezaji akashikamana kwa nguvu katika Maandiko. “Desturi,” akasema, “haina uwezo katika Usuisi wetu, isipokuwa kwa sheria; sasa katika mambo ya imani, Biblia ndiyo sheria yetu.”TSHM 84.4

    Utulivu, kutumia akili kwa Mtengenezaji, unyenyekevu na adabu ulioonyeshwa, ikavuta mafikara na watu wakachukia majivuno ya kiburi cha Eck.TSHM 84.5

    Mabishano yakaendelea kwa mda wa siku kumi na mnane. Wakatoliki wakadai ushindi. Kwa namna wajumbe wengi walikuwa wa upande wa Roma, na baraza ikatangaza kwamba Watengenezaji walishindwa na pamoja na Zwingli, waondoshwe kanisani. Lakini mashindano yakatokea katika mvuto wa nguvu kwa ajili ya Waprotestanti. Baada ya mda mfupi tu, miji mikubwa ya Berne na Bâ le ikajitangaza kuwa kwa upande wa Matengenezo.TSHM 84.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents