Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ushindi kwa Ajili ya Matengenezo

    Ndizo zilikuwa njia ambazo Roma ilitumia kuzima nuru ya Matengenezo, kwa kuondolea watu Neno la Mungu, na kwa kuimarisha ujinga na ibada ya sanamu ya Miaka ya Giza. Lakini chini ya mibaraka ya Mungu na kazi za watu bora ambao aliinua kwa kufuata Luther, dini ya Kiprotestanti haikukomeshwa. Si kwa wema ao kwa silaha za wafalme ambaye iliweza kupata nguvu zake. Inchi ndogo sana na mataifa zaifu zaidi yakawa ngome zake. Ilikuwa Geneve ndogo; ilikuwa Hollande, kushindana juu ya ukorofi wa Espagne; ilikuwa Suede ya ukiwa na ukame, ambazo zilipata ushindi kwa ajili ya Matengenezo.TSHM 109.2

    Karibu miaka makumi tatu Calvin alitumika Geneve kwa ajili ya maendeleo ya Matengenezo pote katika Ulaya. Mwenendo wake haukuwa bila kosa, wala mafundisho yake kukosa kuwa na makosa. Lakini alikuwa chombo cha kutangaza ukweli ya maana ya kipekee; katika kuimarisha dini ya Kiprotestanti juu ya mwendo wa kurudi kwa upesi kufaulu kwa kanisa la Papa, na kwa ajili ya kuingiza katike makanisa ya Matengenezo unyofu na usafi wa maisha.TSHM 109.3

    Kutoka Geneve, wakaenda kutangaza mafundisho ya Matengenezo. Hapo, inchi zote za watu walioteswa wakatafuta kupata mafundisho na kutiwa moyo. Mji wa Calvin ukawa kimbilio la Watengenezaji waliowindwa katika Ulaya yote ya Magharibi. Wakakaribishwa vizuri na kutunzwa vizuri sana; na wakapata makao pale, wakaletea mji uliowapokea mibaraka ya ufundi wao, elimu yao, na utawa wao. John Knox, Mtengenezaji hodari wa Scotland (Ecosse), si hesabu ndogo ya watu wanyofu wa Uingereza, Waprotestanti wa Hollande na wa Espagne, na wa Huguenots wa Ufaransa, wakachukua kutoka Geneve mwenye wa ukweli kuangazia giza kwa inchi zao za kuzaliwa.TSHM 109.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents