Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  30 / SHETANI NA MTU KATIKA VITA

  “Na nitatia uadui katikati yako na mwanamuke, na katikati ya uzao wako na uzao wake; ataponda kichwa chako, na wewe utaponda kisingino chake.” Mwanzo 3:15. Uadui huu si wa tangu awali. Wakati mtu alipovunja sheria ya Mungu, hali yake ikawa mbaya, katika umoja na Shetani. Malaika walioanguka na watu wabaya wakajiunga katika urafiki wa kutokuwa na matumaini. Kama Mungu hakujitia kati, Shetani na mtu wangaliingia katika mapatano kumpinga Mungu wa mbinguni, na jamaa lote la binadamu lingalijiunga katika upinzanii kwa Mungu.TSHM 246.1

  Wakati Shetani aliposikia kwamba uadui ulipashwa kuwa kati yake na mwanamuke, na kati ya uzao wake na uzao wa mwanamuke, alijua kwamba kwa sababu yo yote mtu alipashwa kuwa mtu asiyeweza kupinga uwezo wake.TSHM 246.2

  Kristo alitia uadui ndani ya mtu kumpinga Shetani. Pasipo neema hii ya kugeuka na nguvu inayomfanya mpya, mtu angaliendelea kuwa mtumishi tayari daima kufanya mapenzi ya Shetani. Lakini kanuni mpya katika nafsi inaleta vita; uwezo ambao Kristo anatoa unawezesha mtu kushindana na mkorofi mkuu. Kuchukia sana zambi badala ya kuipenda kunaonyesha kanuni kabisa kutoka juu.TSHM 246.3

  Uadui kati ya Kristo na Shetani ulionekana wazi namna dunia ilivyompokea Yesu. Usafi na utakatifu wa Kristo uliamsha juu yake uchuki wa wasiomuogopa Mungu. Kujikana kwake kulikuwa laumu la duhakikisho kwa wenye kiburi na wapenda anasa ya mwili. Shetani na malaika wabaya wakaungana na watu wabaya kupinga ya Mshindi wa kweli. Uadui wa namna moja unaonyeshwa kwa wafuasi wa Kristo. Ye yote anayesimama imara kwa jaribu ataamsha hasira ya Shetani. Kristo na Shetani hawawezi kupatana. Na wote wanaotaka kuishi maisha ya utawa katika Kristo Yesu watapata mateso.” 2 Timoteo 3:12.TSHM 246.4

  Wajumbe wa Shetani wanatafuta kudanganya wafuasi wa Kristo na kuwavuta kwa utii wao. Wanapotosha Maandiko kwa kutirniza kusudi lao. Roho iliyotia Kristo kwa mauti inaamsha waovu kuharibu wafuasi wake. Yote hii inaonyeshwa mbele katika ule unabii wa kwanza: “Na nitatia uadui katikati yako na mwanamuke, na katikati ya uzao wako na uzao wake.”TSHM 246.5

  Sababu gani Shetani hakutani na ushindani mkubwa? Kwa sababu askari za Kristo wanakuwa na uhusiano mdogo sana pamoja na Kristo. Zambi haiwachukizi kama ilivyomchukiza Bwana wao. Hawajitoi kwa kupigana nayo. Tabia ya mkuu wa giza imewafanya vipofu. Wengi hawajui kwamba adui wao ni mkubwa mwenye nguvu za kupigana kumpinga Kristo. Hata wahuduma wa habari njema hawaoni ushaihidi wa kazi yake. Wanaonekana kutojali kuwako kwa hakika kwake.TSHM 246.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents