Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ingeweza kuwa Nini

  Kukimbia kwa Wahuguenots,ufungufu na inchi nzima ukawa katika Ufransa. Miji ya usitawi kwa viwanda ikaanguka kwa uharibifu. ... Ikakadirishwa kwamba, kwa mwanzo wa Mapinduzi, maelfu mia mbili ya wamaskini katika Paris wakadai mapendo kwa mikono ya mfalme. Wajesuites peke yao walifanikiwa katika taifa lililoharibika.”TSHM 131.1

  Injili ingalileta suluhu kwa magumu hayo yaliyoshinda mapadri wake, mfalme, na wafanya sheria, na mwishowe wakaingiza taifa katika uharibifu. Lakini chini ya utawala wa Roma watu wakapoteza mafundisho ya Mwokozi ya kujinyima na upendo wa choyo kwa ajili ya mazuri ya wengine. Mtajiri hakuwa na karipio kwa ajili yakugandamiza maskini; maskini hawakuwa na msaada kwa uzaifu wao. Choyo ya mtajiri na uwezo yakazidi kulemea. Kwa karne nyingi, watajiri wakakosea wamaskini, na wamaskini wakawachukia matajiri.TSHM 131.2

  Katika majimbo mengi madaraka ya wafanyakazi yalikuwa chini ya wenyeji na walilazimishwa kutii maagizo ya kupita kiasi. Madaraja ya katikati na ya chini ya wafanya kazi wakalipishwa kodi ya nguvu kwa watawala wa serkali na wa dini. “Wakulima na wakaaji wa vijiji waliweza kuteswa na njaa, kwani watesi wao hawakujali. ... Maisha ya watumikaji wakulima yalikuwa ya kazi isiyokuwa na mwisho na taabu isiyokuwa na kitulizo; maombolezo yao ... yaiizaniwa kuwa zarau ya ushupavu. ... Mambo mabaya ya rushwa yakakubaliwa kwa hakika na waamzi. ... Ya kodi, ... nusu ya feza ikaenda kwa hazina ya mfalme ao ya askofu; inayobaki ikatumiwa ovyo ovyo katika anasa ya upotovu. Na watu waliozoofisha hivi wenzao wakaachiliwa wenyewe bila kulipa kodi na walikuwa na haki kwa sheria ao kwa desturi, kwa maagizo yote ya serkali. ... Kwa ajili ya furaha yao mamilioni walihukumiwa maisha mabaya bila tumaini.” (Tazama Nyongezo.)TSHM 131.3

  Zaidi ya nusu ya karne mbele ya Mapinduzi kiti cha ufalme kilikaliwa na Louis XV, aliyetambulika nakuwa mfalme mvivu, asiyejali, na waanasa. Kwa habari ya feza ya serkali wakawa na matatizo na watu wakakasirishwa, haikuhitajiwa jicho la nabii kuona maasi makali. Ilikuwa vigumu kuharakisha hoja ya kufanya matengenezo. Ajali iliyongojea Ufransa ilielezwa katika jibu la kujipenda ama choyo cha mfalme, “Baada yangu, garika!”TSHM 131.4

  Roma ilivuta wafalme na vyeo vya watawala kuweka watu katika utumwa, kukusudia kufunga wote watawala na watu katika vifungo vyake vya minyororo juu ya roho zao. Huku hali mbaya ya tabia njema ambayo ni matokeo ya siasa hii ilikuwa ya kutisha zaidi mara elfu kuliko mateso ya kimwili. Kukosa Biblia, na kujitia katika kujipendeza, watu wakajifunika katika ujinga na kuzama katika maovu, kabisa hawakuweza kujitawala.TSHM 131.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents