Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Wahubiri Watoto wa Skandinavie

    Katika Skandinavie vilevile ujumbe wa kurudi kwa Yesu alitangazwa. Wengi wakasimama kutubu na kuacha zambi zao na kutafuta rehema katika jina la Kristo. Lakini padri wa kanisa la mahali pale akapinga mabadiliko, na wengine waliohubiri ujumbe wakatupwa gerezani.TSHM 175.4

    Mahali pengi ambapo wahubiri wa kuja kwa Bwana kwa karibu walinyamazishwa, Mungu akapendezwa kutuma ujumbe kwa njia ya watoto wadogo. Kama vile walikuwa chini ya umri wa maisha ya mtu mzima, serkali haikuweza kuwafunga, na wakaruhusiwa kusema bila kusumbuliwa.TSHM 175.5

    Katika makao yake ya umasikini watu wakakusanyika kusikia maonyo. Wahubiri wengine watoto hawakuwa zaidi ya umri wa miaka sita ao mnane; ijapo maisha yao yalishuhudia kwamba walimpenda Mwokozi, wakaonyesha tu kwa kawaida akili na uwezo vinavyoonekana katika watoto wa umri ule. Wakati waliposimama mbele ya watu, lakini, walibadilishwa na mvuto mbali ya zawadi zao za kawaida. Sauti na tabia vikageuka, na pamoja na uwezo mkubwa wakatoa maonyo ya hukumu, “Ogopeni Mungu, na kumutukuza kwa maana saa ya hukumu yake imekuja.”TSHM 176.1

    Watu wakasikiliza kwa kutetemeka. Roho wa Mungu akasema mioyoni. Wengi wakaongozwa kwa kutafuta Maandiko, wasiokuwa na kiasi wakatengenezwa, na kazi ikafanywa kwa kuonyesha kwamba hata wachungaji wa kanisa la pale walilazimishwa kukubali kwamba mkono wa Mungu ulikuwa katika mabadiliko.TSHM 176.2

    Ilikuwa mapenzi ya Mungu kwamba habari ya kuja kwa Mwokozi ilipashwa kutolewa katika Skandinavie, na akaweka Roho yake juu ya watoto ili kazi iweze kutendeka. Wakati Yesu alipokaribia Yerusalema, watu, wakaogopeshwa na mapadri na watawala, wakaacha tangazo lao la furaha walipokuwa wakiingia kwa milango ya Yerusalema. Lakini watoto katika viwanja vya hekalu wakachukua kiitikio, na wakapaaza sauti, “Hosana kwa Mwana wa Daudi!” Matayo 21:8-16. Kwa namna Mungu alitenda kazi kwa njia ya watoto kwa wakati wa kuja kwa mara ya kwanza kwa Kristo, ndivyo hivyo akatumika kwa njia yao katika kutoa ujumbe wa kuja kwake kwa mara ya pili.TSHM 176.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents