Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Uwezo Kamili wa Maandiko

    Kanuni kubwa iliyoshikwa na Watengenezaji hawa--ni ile ile iliyoshikwa na Wavaudois, Wycliffe, Huss, Luther, Zwingli, na wafuasi wao--ni uwezo kamilifu wa Maandiko matakatifu. Kwa mafundisho yake wakajaribu mafundisho ya dini yote na madai yote. Ni imani katika Neno la Mungu iliyosaidia watu hawa watakatifu walipotoa maisha yao kwa kigingi. “Muwe wakufarijika,” akasema Latimer kwa wenzake wafia dini wakati sauti zao zilikuwa karibu kunyamazishwa na ndimi za moto, “tutawasha leo mshumaa, kwa neema ya Mungu, katika Uingereza, jinsi ninavyo tumaini hautazimika.”TSHM 115.6

    Kwa mamia ya miaka baada ya makanisa ya Uingereza yalipotii mamlaka ya Roma, wale wa Scotland (Ecosse) wakashika uhuru wao. Kwa karne ya kumi na mbili, hata hivyo, dini ya papa ikaimarishwa katika inchi, na sehemu zote zikafunikwa na giza nzito. Lakini miali ya nuru ikaja kuangazia giza hiyo. Wa Lollards, kutoka Uingereza pamoja na Biblia na mafundisho ya Wycliffe, wakafanya mengi kwa kulinda maarifa ya injili. Kwa kufunguliwa kwa Matengenezo kukaja maandiko ya Luther na Agano Jipya la Kingereza la Tyndale. Wajumbe hawa kwa ukimya wakapitia milimani na katika mabonde, wakawasha katika maisha mapya mienge ya kweli iliyokuwa karibu kuzimika na kufanya upya tena kazi ambayo iligandamizwa na karne inne za mateso.TSHM 116.1

    Ndipo waongozi wa kanisa la Papa, mara wakaamshwa kwa hatari iliyohofisha kazi yao, wakapandisha watoto wengi wa watu bora wa Scotland (Ecosse) kwa kigingi. Washahidi hawa waliokufa po pote katika inchi wakafurahisha roho za watu na kusudi isiyokufa ya kuvunja minyororo za Roma.TSHM 116.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents