Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Tunda la Mafundisho Mapya Limeonekana (limetambulika)

  Watu wakaongozwa kuzarau Biblia ao kuikataa yote kabisa. Wanafunzi wakaacha mafundisho yao na kutoka kwa chuo kikubwa. Watu waliojizania kwamba ni wenye uwezo kwa kurudisha nafsi na kuongoza kazi ya Matengenezo wakafaulu tu kuileta katika uharibifu. Sasa Wakatoliki wakapata tumaini lao, nakulalamika kwa furaha. “Juhudi ya mwisho tena, na wote watakuwa wetu.”TSHM 86.2

  Luther huko Wartburg, aliposikia mambo yaliyotendeka, akasema na masikitiko sana: “Nilifikiri wakati wowote kwamba Shetani angetumia mateso haya.” Akatambua tabia ya kweli ya wale waliojidai kuwa “manabii.” Upinzani wa Papa na mfalme haukumletea mashaka makubwa sana na shida kama sasa. Miongoni mwa waliojidai kuwa “rafiki” za Matengenezo, kukatokea adui zake wabaya kuliko kwa kuamsha vita na kuleta fujo.TSHM 86.3

  Luther aliongozwa na Roho wa Mungu na kupelekwa mbali ya kujisikia binafsi. Huku kila mara alikuwa akitetemeka kwa matokeo ya kazi yake: “Kama ningelijua kwamba mafundisho yangu yaliumiza mtu mmoja, mtu mmoja tu, ingawa mnyenyekevu na mnyonge-lisipoweza kuwa, kwani linakuwa ni injili yenyewe--ningekufa mara kumi kuliko mimi kuikana.”TSHM 86.4

  Wittenberg yenyewe ilikuwa ikianguka chini ya mamlaka ya ushupavu wa dini isiyo ya akili na machafuko. Katika Ujeremani pote adui za Luther wakatwika mzigo huo juu yake. Katika uchungu wa roho akajiuliza, “Je, ni hapo basi kazi hii kubwa ya Matengenezo ilipaswa kumalizikia?” Tena, kama vile alikuwa akishindana na Mungu katika sala, amani ikaingia moyoni mwake. “Kazi si yangu, bali ni yako mwenyewe,” akasema. Lakini akakusudia kurudi Wittenberg.TSHM 86.5

  Alikuwa chini ya laana ya ufalme; Adui zake walikuwa na uhuru wa kumuua, rafiki walikatazwa kumlinda. Lakini aliona kwamba kazi ya injili ilikuwa katika hatari, na katika jina la Bwana akatoka bila uwoga kupigana kwa ajili ya ukweli. Ndani ya barua kwa mchaguzi, Luther akasema: “Ninaenda Wittenberg chini ya ulinzi wa yule anayekuwa juu kuliko ule wa wafalme na wachaguzi. Sifikiri kuomba usaada wa fahari yako, wala kutaka ulinzi wako, ningependa kukulinda mimi mwenyewe. ... Hakuna upanga unaoweza kusaidia kazi hii. Mungu peke yake anapashwa kufanya kila kitu.” Katika barua ya pili, Luther akaongeza: “Niko tayari kukubali chuki ya fahari yako na hasira ya ulimwengu wote. Je, wakaaji wa Wittenberg si kondoo zangu? Na hainipasi, kama ni lazima, kujitoa kwa mauti kwa ajili yao?”TSHM 86.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents