Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Jaribu Kubwa la Uaminifu

  Sabato, jaribu kubwa la uaminifu, ni ukweli hasa unaopingwa. Huku kushika sabato ya uwongo kutakuwa neno la kukiri la utii kwa mamlaka yanayo mpinga Mungu, kushika kwa Sabato ya kweli ni ushahidi wa uaminifu kwa Muumba. Wakati kundi moja linapopokea alama ya nyama, lingine hupokea muhuri wa Mungu.TSHM 295.2

  Maonyo ya kwamba kukosa uvumulivu wa dini kungepata utawala, ya kama kanisa na serkali wangetesa wale wanaoshika amri za Mungu, yangetangazwa pasipo sababu na kwa upuzi. Lakini kwa namna kushika kwa siku ya kwanza (dimanche) kunatikiswa mahali pengi sana, jambo lililokuwa halikusadikiwa kwa wakati mrefu linaonekana kuwa karibu, na ujumbe utaleta tukio ambalo lisingaliweza kuwako mbele.TSHM 295.3

  Katika kila kizazi Mungu ametuma watumishi wake kukemea zambi ulimwenguni na katika kanisa. Watengenezaji (réformateurs) wengi, kwa kuingia kwa kazi yao, wakakusudia kutumia busara nyingi katika kushambulia zambi za kanisa na za taifa. Wakatumainia, kwa mfano wa maisha safi ya Kikristo, kuongoza watu kurudi kwa Biblia. Lakini Roho wa Mungu akaja juu yao; pasipo hofu ya matokeo, hawakuweza kuzuia kuhubiri mafundisho zahiri ya Biblia.TSHM 295.4

  Kwa hivyo ujumbe utatangazwa. Bwana atatumika kwa njia ya vyombo vinyenyekevu vinavyojitia wakuf wenyewe kwa kazi yake. Watumukaji watastahilishwa zaidi kwa kupakwa mafuta ya roho Mtakatifu kuliko kwa mafundisho ya vyama vya vitabu. Watu watalazimishwa kuendelea mbele na juhudi takatifu , kutangaza maneno ambayo Mungu anayotoa. Zambi za Babeli zitafunuliwa. Watu watashitushwa. Maelfu hawajasikia kamwe maneno kama haya. Babeli ni kanisa, lililoanguka kwa sababu ya zambi zake, kwa sababu ya kukataa kwake kwa ukweli. Jinsi vile watu wanavyo kwenda kwa walimu wao na maswali “je, mambo haya ni hivyo”? Wahubiri wanaonyesha mifano kwa kutuliza zamiri iliyoamshwa. Lakini kwa namna wengi wanapouliza zahiri “Bwana anasema hivi”, kazi ya mapadri ya watu wengi itaamsha makutano yanayopenda zambi kwa kutukana na kutesa wale wanao tangaza.TSHM 295.5

  Mapadri watatumia juhudi zaidi za kupita uwezo wa kibinada-mu kwa kufungia mbali nuru, kwa kuzuia mabishano ya maswali haya ya maana sana. Kanisa linaomba kwa mkono hodari wa mamlaka ya serikali, na katika kazi hii, wafuasi wa kanisa la kiroma na waprotestanti huungana. Kwa namna mwenendo wa mkazo wa siku ya kwanza (dimanche) unapokuwa wa nguvu zaidi, washikaji wa amri watatishwa kwa kulipa feza na kifungo. Wengine wanatolewa vyeo vya mvuto na wengine zawadi zingine kwa kukana imani yao. Lakini jibu lao ni “Mtuonyeshe kutoka katika Neno la Mungu kosa letu”. Wale walioshitakiwa mbele ya baraza wanafanya ushuhuda wa nguvu wa ukweli, na wengine wanaowasikia huongozwa kwa kukata shauri la kushika amri zote za Mungu. Kama sivyo maelfu hawangeweza kujua kitu juu ya mambo haya ya kweli.TSHM 296.1

  Utii kwa Mungu ungetendewa kama uasi. Mzazi atatumia ukali kwa mtoto mwenye kuamini. Watoto wataondolewa katika urithi na kufukuzwa kutoka nyumbani. “Na wote wanaotaka kuishi maisha ya utawa katika Kristo Yesu watapata mateso”. 2 Timoteo 3:12. Kuwa kama wateteaji wa ukweli wanapokataa kuheshimu siku ya kwanza (dimanche) wengine wataingizwa gerezani, wengine watahamishwa, wengine watatendewa kama watumwa. Kwa namna roho ya Mungu atakavyoondolewa kutoka kwa watu hapo kutakuwa maendeleo ya kigeni. Moyo unaweza kuwa na jeuri sana wakati uchaji wa Mungu na upendo yanapoondolewa.TSHM 296.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents