Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  19 / SABABU GANI UCHUNGU MKUBWA ULE?

  Kazi ya Mungu huonyesha mwaka kwa mwaka, mfano wa kutisha kila matengenezo makubwa ao mwenendo wa dini. Kanuni za matengenezo ya Mungu kuhusu watu yanakuwa mamoja daima. Mabadiliko makubwa ya sasa yanakuwa na uhusiano na yale ya wakati uliopita, na maarifa ya kanisa katika vizazi vya kwanza yanakuwa na mafundisho kwa wakati wetu.TSHM 164.1

  Mungu kwa Roho Mtakatifu wake kwa upekee huongoza watumishi wake duniani katika kuepeleka mbele kazi ya wokovu. Watu ni vyombo katika mkono wa Mungu. Kwa kila chombo kulitolewa sehemu ya nuru ya kutosha kwa kumwezesha kufanya kazi aliyopewa kufanya. Lakini hakuna mtu kamwe aliyefikia ufahamu kamili wa kusudi la Mungu katika kazi kwa wakati wake mwenyewe. Watu hawafahamu kabisa katika uchukuzi wake wote ujumbe ambao wanaoutoa katika jina lake. Hata manabii hawakufahamu kabisa mambo ya ufunuo yaliyotolewa kwao. Maana ya ufunuo ilikuwa ya kufunuliwa toka kizazi kwa kizazi. Petro anasema: “Katika habari za wokovu huu manabii walitafuta na kuchunguza, wao waliotabiri juu ya neema itakayowafikia ninyi; walichunguza nini ao wakati wa namna gani Roho ya Kristo aliyekuwa ndani yao aliwaonyesha wakati aliposhuhudia mbele mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakao yafuata. Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe lakini ni kwa ajili yetu waliohudumiwa.” 1 Petro 1:10-12, Ni sisi herufi tofauti(italics). Fundisho la namna gani kwa watu wa Mungu katika kizazi cha ukristo! Watu hao “watakatifu wa Mungu” walitafuta na kuchunguza “kwa bidii” kwa ajili ya mafunuo zilizotolewa kwa vizazi ingawa vilikuwa havijazaliwa bado. Kemeo gani kwa ukavu wa macho wa wapenda dunia ambayo wanatosheka kutangaza kwamba mambo ya unabii hayawezi kufahamiwa.TSHM 164.2

  Si mara chache mafikara hata ya watumishi wa Mungu yanakuwa ya kupofushwa sana kwa manebo ya asili na mafundisho ya uwongo ambayo wanashika kwa nusu tu mambo yaliyofunuliwa katika Neno la Mungu. Wanafunzi wa Kristo, hata wakati Mwokozi alikuwa pamoja nao, walikuwa na wazo la kupendwa na watu wote juu ya Masiya kama mfalme wa mda aliyepashwa kuinua Israel; kwa mamlaka ya wakati wote. Hawakuweza kufahamu maneno yake yaliyotabiri mateso na mauti yake.TSHM 164.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents