Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    26 / WASHUJAA KWA AJILI YA UKWELI

    Matengenezo juu ya sabato katika siku za mwisho yametabiriwa katika Isaya: “Bwana anasema hivi: Shikeni hukumu, na mufanye haki; kwa sababu wokovu wangu ni karibu kuja, na haki yangu kufunuliwa. Heri mtu anayefanya maneno haya, na mwana wa mtu anayeyashika sana; anayeshika sabato asizivunje, anayezuiza mkono wake usifanye uovu wo wote... Vilevile wana wa mgeni, wanaojiunga na Bwana, kumutumikia, na kupenda jina la Bwana, kuwa watumishi wake, yeyote anayeshika sabato asiivunje, na kushika sana agano langu; hata wale nitawaleta kwa mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya maombi.” Isaya 56:1,2,6,7.TSHM 219.1

    Maneno haya yanaelekea kwa wakati wa kikristo, kama inavyoonyeshwa kwa maneno (mstari 8). Hapa ni kuonyesha mbele mkusanyiko wa Mataifa kwa njia ya habari njema, wakati watumishi wake wanapohubiri kwa mataifa yote habari za furaha.TSHM 219.2

    Bwana anaamuru, “Tia muhuri juu ya sheria katikati ya wanafunzi wangu.: Isaya 8:16. Muhuri wa sheria ya Mungu unapatikana katika amri ya ine. Hii tu, ya amri zote kumi, inayoleta maoni ya jina na anwani ya Mutoa sheria. Wakati Sabato ilipogeuzwa kwa mamlaka ya Papa (kanisa la Roma), muhuri uliondolewa kutoka kwa sheria. Wanafunzi wa Yesu wanaitwa kwa kuurudisha kwa kuinua Sabato kama ukumbusho wa Muumba na alama ya mamlaka yake.TSHM 219.3

    Agizo limetolewa: “Piga kelele, usiache, pandisha sauti yako kama baragumu, uhubiri watu wangu kosa lao.” Wale ambao Bwana anawataja kama “watu wangu” wanapaswa kukaripiwa kwa ajili ya makosa yao, kundi linalojifikiri wao wenyewe kuwa la haki katika kazi ya Mungu. Lakini kemeo la upole la mwenye kutafuta mioyo linawashuhudia kuvunja amri za Mungu. Isaya 58:1,2.TSHM 219.4

    Kwa hiyo nabii anaonyesha amri ambayo iliyoachwa: “Utanyanyulisha misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza pahali pa kubomoka; Mwenye kurudisha njia za kukalia. Kama ukigeuza mguu wako kutoka katika Sabato, usifanye mapenzi yako katika siku yangu takatifu na kuita sabato siku ya furaha, siku takatifu ya Bwana, yenye heshima; kama ukiiheshimu, pasipo kufuata njia zako mwenyewe, wala kutafuta mapenzi yako mwenyewe, wala kusema maneno yako mwenyewe; ndipo utajifurahisha katika Bwana.” Isaya 58:12-14.TSHM 219.5

    “Tundu” lilifanywa katika sheria ya Mungu wakati Sabato ilipogeuzwa kwa mamlaka ya Roma. Lakini wakati umefika kwa tundu kutengenezwa.TSHM 219.6

    Sabato ilishikwa na Adamu katika usafi wake katika Edeni; na Adamu, aliyeanguka lakini akatubu, wakati alipofukuzwa kwa shamba ao cheo chake. Ilishikwa na mababa wote tangu Abeli hata Noa, kwa Abrahamu, hata Yakobo. Wakati Bwana alipookoa Israeli, akatangaza sheria yake kwa makutano.TSHM 220.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents