Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Nani Atakayesimama?

  Nabii akasema: “Nani atakayevumilia siku ya kuja kwake? na nani atakayesimama wakati atakapoonekana? ... Naye atakaa kama mwenye kusafisha na kutakasa feza, naye atatakasa wana wa Lawi, na atawasafisha kama zahabu na feza, nao watatoa kwa Bwana sadaka kwa haki.” Malaki 3:2,3. Wale wanaokaa duniani wakati teteo ya Kristo yatakapoisha wanapashwa kusimama mbele ya Mungu bila muombezi. Mavazi yao yanapashwa kuwa safi bila doa, tabia zao zenye kutakaswa kutoka zambini kwa damu ya manyunyu. Kwa njia ya neema ya Mungu na juhudi yao wenyewe ya utendaji wanapashwa kuwa washindaji katika vita na yule muovu. Wakati hukumu ya ukaguzi inapoendelea mbele kule mbinguni, wakati zambi za waamini waliotubu zinapoondolewa kutoka kwa Pahali patakatifu, hapo panapashwa kuwa na kazi ya kipekee ya kuacha zambi miongoni mwa watu wa Mungu duniani. Kazi hii inaonyeshwa katika ujumbe wa Ufunuo 14. Wakati kazi hii itakapotimizwa, wafuasi wa Kristo watakuwa tayari kwa kutokea kwake. Ndipo kanisa ambalo Bwana wetu kwa kuja kwake analopashwa kupokea litakuwa “kanisa la utukufu, pasipo doa wala kikunjo wala kitu cho chote kama hivi.” Waefeso 5:27.TSHM 204.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents