Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Luther Anasimama Mbele ya Baraza

  Mfalme akaketi kitini, anapozungu kwa na watu wa cheo wenye sifa katika ufalme. Martin Luther sasa alipashwa kujibu kwa ajili ya imani yake. “Kuonekana huku kulikuwa kwenyewe ishara (alama) ya ushindi juu ya cheo cha Papa. Papa alimhukumu mtu huyu, na mtu huyu alisimama mbele ya baraza ya hukumu iliyowekwa juu ya Papa. Papa alimweka chini ya makatazo, akakatiwa mbali ya chama cha kibinadamu, na huku akaalikwa katika manemo ya heshima, na kupokelewa mbele ya mkutano wa heshima sana katika ulimwengu. ... Roma ilikuwa ikishuka kutoka kitini chake, nailikuwa ni sauti la mtawa lililomushusha.”TSHM 69.3

  Mzaliwa mnyenyekevu Mtengenezaji akaonekanamwenye kutishwa na kufazaika. Wafalme wengi, wakamkaribia, na mmoja akamnongoneza “Musiwaogope wanaoua mwili lakini hawawezi kuua nafsi.” Mwengine akasema: “Na mutakapopelekwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, mtapewa kwa njia ya roho wa baba yenu lile mtakalo lisema.” Tazama Matayo 10:28, 18, 19.TSHM 70.1

  Ukimya mwingi ukawa juu ya mkutano uliosongana. Ndipo afisa mmoja wa mfalme akasimama na, kushota kwa maandiko ya Luther, akauliza kwamba Mtengenezaji ajibu maswali mawili-ao atayakubali kwamba ni yake, na ao atakusudia kukana mashauri yanayoandikwa humo. Vichwa vya vitabu vilipokwisha kusomwa, Luther, kwa swali la kwanza, akakubali vitabu kuwa vyake. “Kwa swali la pili,” akasema, ningetenda bila busara kama ningejibu bila kufikiri. Ningehakikisha kidogo kuliko hali ya mambo inavyotaka, ao zaidi kuliko kweli inavyotaka. Kwa sababu hiyo ninaomba mfalme mtukufu, kwa unyenyekevu wote, unitolee wakati, ili nipate kujibu bila kukosa juu ya neno la Mungu.”TSHM 70.2

  Luther akasadikisha makutano kwamba hakutenda kwa hasira ao bila kufikiri. Utulivu huu, na kujitawala, isiyotazamiwa kwa mtu aliyejionyesha kuwa mgumu na asiyebadili shauri yakamwezesha baadaye kujibu kwa busara na heshima ikashangaza maadui zake na kukemea kiburi chao.TSHM 70.3

  Kesho yake alipashwa kutoa jibu lake la mwisho. Kwa mda moyo wake ukadidimia. Maadui zake walionekana kwamba wangeshinda. Mawingu yakakusanyika kando yake na yakaonekana kumtenga na Mungu. Katika maumivu ya roho akatoa malalamiko yale ya kuhuzunisha sana, ambayo Mungu tu anaweza kuyafahamu kabisa.TSHM 70.4

  “Ee Mwenyezi Mungu wa milele!” akapaza sauti; “kama ni kwa nguvu za ulimwengu huu tu ambapo napashwa kutia tumaini langu, yote imekwisha. ... Saa yangu ya mwisho imefika, hukumu yangu imekwisha kutangazwa. ... Ee Mungu, unisaidie juu ya hekima yote ya ulimwengu. ... Mwanzo ni wako, ... na ni mwanzo wa haki na wa milele. Ee Bwana, unisaidie! Mungu mwaminifu na asiyebadilika, mimi si mtumainie mtu ye yote. ... Umenichagua kwa kazi hii. ... Simama kwa upande wangu, kwa ajili ya jina la mpendwa wako Yesu Kristo, anayekuwa mkingaji wangu, ngao yangu, na mnara wangu wa nguvu.”TSHM 70.5

  Lakini haikuwa hofu ya mateso, maumivu, wala mauti yake mwenyewe ambayo ilimlemea na hofu kuu. Alijisika upungufu wake. Katika uzaifu wake madai ya ukweli yangeweza kupata hasara. Si kwa usalama wake mwenyewe, bali kwa ajili ya ushindi wa injili alishindana na Mungu. Katika ukosefu wa usaada imani yake ikashikilia juu ya Kristo, Mkombozi mkuu. Hangeonekana pekee yake mbele ya baraza. Amani ikarudi kwa roho yake, na akafurahi kwamba aliruhusiwa kuinua Neno la Mungu mbele ya watawala wa mataifa.TSHM 71.1

  Luther akawaza juu ya jibu lake, akachunguza maneno katika maandiko yake, na akapata kwa Maandiko matakatifu mahakikisho ya kufaa kwa kusimamia maneno yake. Ndipo, akatia mkono wake wa kushoto kwa Kitabu Kitakatifu, akainua mkono wake wa kuume mbinguni na akaapa kwa kiapo “kukua mwaminifu kwa injili, na kwa uhuru kutangaza imani yake, hata ingeweza kutia mhuri kwa ushuhuda wake kwa kumtia damu yake.”TSHM 71.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents