Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Makundi ya Malaika Wanalinda

    Malaika wanatua kwa wale waliolinda neno la uvumilivu la Kristo. Wameshuhudia shida yao na wamesikia maombi yao. Wanangojea neno la Mkuu wao kuwanyakua kwa hatari yao. Lakini wanapashwa kungojea wakati mrefu kidogo. Watu wa Mungu wanapashwa kunywa kikombe na kubatizwa kwa ubatizo. Matayo 20:20-23. Lakini kwa ajili ya wateule wakati wa taabu utafupishwa. Mwisho utakuja upesi kuliko watu wanavyotazamia.TSHM 306.5

    Ingawa amri ya kawaida imeweka wakati washika amri wanapoweza kuuawa, adui zao kwa sababu zingine wataharakisha amri na kujaribu kuondoa maisha yao. Lakini hakuna mtu anayeweza kupita walinzi waliotua kuzunguka kila nafsi aminifu. Wengine walishambuliwa wakati wa kukimbia kwao kutoka mijini, lakini panga zilizoinuliwa juu yao zikavunjika kama majani makavu. Wengine wakalindwa na malaika katika hali ya watu wa vita.TSHM 307.1

    Katika vizazi vyote viumbe vya mbinguni wamekamata sehemu ya juhudi katika mambo ya watu. Wamekubali kukaribisha na wanadamu, kutenda kama viongozi kwa wasafiri wajinga, wakafungua milango ya gereza na kuweka huru watumishi wa Bwana. Wakaja kusukuma jiwe kwa kaburi la Mwokozi.TSHM 307.2

    Malaika wanazuru mikutano ya waovu, kama walivyokwenda Sodomo, kuhakikisha kama wamepitisha mpaka wa uvumilivu wa Mungu. Bwana, kwa ajili ya wachache wanamtumikia kwa kweli, anazuia misiba na anazidisha utulivu wa makutano. Wenye zambi wanafahamu kidogo sana ya kwamba wandeni kwa maisha yao juu ya waaminifu wachache ambao wanafurashwa kwa kuwagandamiza.TSHM 307.3

    Kila mara katika baraza za ulimwengu huu, malaika wamekuwa wanenaji. Masikio ya kibinadamu yamesikiliza kwa miito yao, midomo ya kibinadamu yamezihakia mashauri yao. Wajumbe hawa wa mbinguni wametibitisha vyema kuliko wao wenyewe kuweza kutetea kisa cha waliozulumiwa kuliko wateteaji wao wenye uwezo wa kusema vema. Wameshinda na kufunga waovu wale wangeleta mateso kwa watu wa Mungu.TSHM 307.4

    Kwa tamaa ya bidii, watu wa Mungu wanangojea ishara za kuja kwa Mfalme wao. Wakati wale wanaoshindana wanapoendesha maombi yao mbele ya Mungu, mbingu zaangaza na mapambazuko ya siku ya milele. Kama sauti tamu za nyimbo za malaika maneno yanaanguka kwa sikio: “saidia anakuja. ” Sauti ya Kristo inakuja kutoka kwa milango wazi: “Tazama, ninakuwa pamoja nanyi. Msiogope. Nimepigana vita kwa ajili yenu, na katika jina langu munakuwa zaidi kuliko washindaji.”TSHM 307.5

    Mwokozi mpenzi atatuma msaada wakati tunapouhitaji. Wakati wa taabu ni hatari ya kutisha kwa watu wa Mungu, lakini kila mwamini wa kweli anaweza kuona kwa imani upindi wa ahadi ukimzunguka. “Hivi watu waliokombolewa na Bwana watarudi, watafika Sayuni na kuimba; Furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; watapata shangwe na furaha; huzuni na kulia kutakimbia”. Isaya 51:11.TSHM 307.6

    Kama damu ya washuhuda wa Kristo ilimwangika kwa wakati huu, uaminifu wao haungekuwa ushuhuda kusadikisha wengine kwa ajili ya kweli, kwa maana moyo mgumu umefukuza nyuma mawimbi ya rehema hata yasirudi tena. Kama wenye haki wanapashwa sasa kuanguka kuwa mawindo kwa adui zao, ingekuwa ushindi kwa mtawala wa giza. Kristo amesema: “Muje, watu wangu, mwingie ndani ya vyumba vyenu, na kufunga milango yenu nyuma yenu; mujifiche kwa dakika kidogo, hata wakati kasirani hii inapopita. Kwa maana tazama, Bwana anakuja kutoka pahali pake kuazibu wenye kukaa duniani kwa ajili ya uovu wao”. Isaya 26:20,21.TSHM 308.1

    Wokovu utakuwa wa utukufu wa wale waliongojea kwa uvumilivu kwa ajili ya kuja kwake na majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima.TSHM 308.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents