Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    2 / WAKRISTO WA KWANZA -WAAMINIFU NA WA KWELI

    Yesu alifunulia wanafunzi wake maarifa ya watu wake tangu wakati ambao alipaswa kuchukuliwa kutoka kwao, hata kurudi kwake katika uwezo na utukufu. Kuingia ndani sana ya wakati ujao, jicho lake likaona zoruba kali zilipaswa kupiga juu ya wafuasi wake kwa miaka iliyokuwa karibu ya mateso. Tazama Matayo 24:9,21,22. Wafuasi wa Kristo wanapaswa kupitia kwa njia ya namna moja ya laumu na mateso ambayo Bwana wao alipitia. Uadui juu ya Mkombozi wa ulimwengu ulipaswa kuonekana juu ya wote wanaopaswa kuamini jina lake.TSHM 9.1

    Upagani ulifahamu kwamba injili ikishinda, hekalu na mazabahu zake yalipaswa kuondolewa; kwa sababu hii mioto ya mateso ikawashwa. Wakristo walinyanganywa mali zao na kufukuzwa nyumbani mwao. Hesabu kubwa ya wenye cheo na watumwa, watajiri na masikini, wenye elimu na wajinga, waliuawa bila huruma.TSHM 9.2

    Ya kianzia chini ya utawala wa Nero, mateso yakaendelea kwa karne nyingi. Wakristo walitangazwa kwa uongo kuwa ni wao walioleta njaa, tauni, na matetemeko ya inchi. Wachongezi wakasimama tayari, kwa ajili ya faida tu, kwa kusaliti wasio na kosa kama waasi na tauni kwa jamii. Hesabu kubwa wakatupwa kwa nyama wa pori ama kuchomwa wahai katika viwanja vya michezo (amphitheatres). Wengine wakasulubiwa; wengine wakafunikwa na ngozi za nyama wa pori na kusukumwa kwa nguvu katika uwanja (arena) wa kuchezea ili kupasuliwa kwa waimbwa. Kwa siku kuu za wote makutano mengi sana yalikusanyika kwa kufurahisha macho na kusalimia walioumizwa kwa kifo na kuwachekeleya na kushangilia.TSHM 9.3

    Wafuasi wa Kristo walilazimishwa kutafuta maficho katika mahali pa ukiwa na pekee. Chini ya milima inje ya muji wa Roma, vyumba virefu vilifunuliwa katika inchi na miamba kwa maelfu ngambo ya pili ya kuta za mji. Ndani ya makimbilio haya ya chini ya udongo wafuasi wa Kristo wakazika wafu wao, na hapo pia walipaswa kukimbilia, walipozaniwa maovu na kugombezwa, walipata makao. Wengi wakakumbuka maneno ya Bwana wao, kwamba kama wakiteseka kwa ajili ya Kristo, inafaa wafurahi sana. Zawadi yao itakuwa kubwa mbinguni, kwa maana ndivyo walivyotesa manabii waliokuwa mbele yao. Tazama Matayo 5:11,12.TSHM 9.4

    Nyimbo za ushindi zikapanda katikati ya ndimi za moto zenye kutatarika. Kwa imani waliona Kristo na malaika wakiwatazama pamoja na usikizi mwingi sana na kutazama kusimama imara kwao pamoja na kibali. Sauti ikaja kutoka kwa kiti cha enzi cha Mungu: “Uwe mwaminifu mpaka kufa, nami nitakupa taji ya uzima”. Ufunuo 2:10.TSHM 10.1

    Nguvu za Shetani kwa kuharibu kanisa la Kristo kwa mauaji zilikuwa bure. Watumishi wa Mungu waliuawa, lakini injili iliendelea kutawanyika na wafuasi wake kuongezeka. Mkristo mmoja akasema: “Tunazidi kuongezeka kwa hesabu namna munavyozidi kutuuwa, damu ya Wakristo ni mbegu”.TSHM 10.2

    Shetani basi, ili aweze kushinda Mungu alikata shauri ya kusimamisha mwenge wake ndani ya kanisa la Kristo, ili apate ujanja kile alichoshindwa kupata kwa nguvu. Mateso yakakoma. Kwa mahali pake kukawekwa mvuto wa mafanyikio ya kidunia heshima za muda. Waabudu sanamu wakaongozwa kupokea sehemu ya imani ya kikristo, wakikataa mambo ya ukweli yaliyo ya maana . Wakatangaza kumkubali Yesu kama Mwana wa Mungu na kuamini kufa na kufufuka kwake, lakini bila kukubali hali yao ya zambi, na hawakusikia lazima ya kuungama au badiliko la moyo waweze kuungana katika mafikara ya imani katika Kristo.TSHM 10.3

    Sasa kanisa lilikuwa katika hofu ya maangamizo. Kifungo, mateso, moto, na upanga vilikuwa ni mibaraka kwa kulinganisha pamoja na jambo hili. Baadhi ya Wakristo walisimama imara, kutangaza kwamba haikupasa kufanya mapatano. Wengine walikubali kugeuza imani yao. Chini ya vazi ya kondoo ya ukristo unaodaiwa, Shetani alikuwa akijificha yeye mwenyewe ndani ya kanisa, kwa kuchafua au kuharibu imani yao.TSHM 10.4

    Wakristo wengi mwishowe walikubali kushusha kanuni ya imani yao. Na umoja ukafanyika kati ya ukristo na upagani. Ingawa waabudu sanamu walijifanya kuwa washiriki wa makanisa walizidi kujiunga kwa ibada ya sanamu zao, ila tu wakageuza vyombo vya ibada yao kwa sanamu za Yesu, na hata za Maria na watakatifu. Mafundisho mabaya, kawaida za kuabudu mambo ya uchawi, na sherehe za ibada ya sanamu zikaunganishwa katika imani ya kanisa na ibada. Dini ya Kikristo ikaharibika, na kanisa likapoteza utakatifu (usafi) na uwezo wake. Wengine lakini, hawakudanganyika. Waliendelea kushika uaminifu wao kwa Muumba wa ukweli.TSHM 10.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents