Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Prague Ikawekwa Chini ya Makatazo

  Habari zikapelekwa Roma, na Huss akaitwa kwa kuonekana mbele ya Papa. Kutii kungalileta kifo cha kweli. Mfalme na malkia wa Bohemia, chuo kikuu, washiriki wa chuo kikuu, na wakuu wa serkali, wakajiunga katika mwito kwa askofu kwamba Huss aruhusiwe kubaki huko Prague na kujibu kwa njia ya ujumbe. Baadaye, Papa akaendelea kuhukumu nakulaumu Huss, na akatangaza mji wa Prague kuwa chini ya makatazo.TSHM 40.5

  Katika mwaka ule hukumu hii ikatia kofu. Watu walimuzania Papa kama mjumbe wa Mungu, wa kushika funguo za mbingu na jehanamu na kuwa na uwezo kuita hukumu. Iliaminiwa kwamba mpaka ilipaswa kupendeza Papa kutosha laana, wafu wangefungiwa kutoka kwa makao ya heri. Kazi zote za dini zikakatazwa. Makanisa yakafungwa. Ndoa zikaazumishwa katika uwanja wa kanisa. Wafu wakazikwa bila kanuni ndani ya mifereji ao mashambani.TSHM 41.1

  Prague ikajaa na msukosuko. Kundi kubwa ya watu wakalaumu Huss na wakadai kwamba alazimiswe kwenda Roma. Kwa kutuliza makelele, Mtengenezaji akapelekwa kwa mda katika kijiji chake cha kuzaliwa. Hakuacha kazi zake, bali alisafiri katika inchi na kuhubiri makutano ya hamu kubwa. Wakati mwamsho katika Prague ulipotulia, Huss akarudi kuendelea kuhubiri Neno la Mungu. Adui zake walikuwa hodari, lakini malkia na wenye cheo kikuu wengi walikuwa rafiki zake, na watu katika hesabu kubwa wakamfuata.TSHM 41.2

  Huss alisimama peke yake katika kazi yake. Sasa Jerome akajiunga katika matengenezo. Wawili hawa baadaye wakajiunga katika maisha yao, na katika mauti hawakuweza kuachana. Katika watu bora hawa ambao huleta nguvu ya kweli ya tabia, Huss alikuwa mkubwa zaidi. Jerome, kwa kujinyenyekea kwa kweli, akapata thamani yake na kunyenyekea kwa mashauri yake. Chini ya kazi zao za muungano matengenezo yakazambaa kwa upesi.TSHM 41.3

  Mungu akaruhusu nuru kuangaza juu ya akili za watu hawa wateule, kuwafunulia makosa mengi ya Roma, lakini hawakupokea nuru yote ya kutolewa ulimwenguni. Mungu alikuwa akiongoza watu kutoka katika giza ya Kanisa la Roma, na akazidi kuwaongoza, hatua kwa hatua, namna waliweza kuichukua. Kama utukufu wote wa jua la azuhuri kwa wale waliodumu gizani mda mrefu, nuru kamili ingewaletea kurudi nyuma. Kwa hiyo aliifunua kidogo kidogo, jinsi ilivyowezekana kupokelewa na watu.TSHM 41.4

  Matengano katika kanisa likaendelea. Mapapa watatu sasa walikuwa wakishindania mamlaka. Ushindano wao ukajaza jamii ya mataifa ya Wakristo wote machafuko. Hakutoshelewa na kuvurumisha laana, kila mmoja ni kununua silaha na kupata waaskari. Kwa kweli feza ziweko; kwa kupata hizi, zawadi, fazili, na mibaraka ya kanisa yalitolewa kwa ajili ya biashara. (Tazama Nyongezo)TSHM 41.5

  Pamoja na uhodari ulioongezeka Huss akapiga ngurumo juu ya machukizo yaliyo vumiliwa katika jina la dini. Watu wakashitaki Roma wazi wazi kuwa chanzo cha shida iliyoharibu miliki ya kikristo.TSHM 41.6

  Tena Prague ilionekana kukaribia ugomvi wa damu. Kama katika miaka ya zamani, mtumishi wa Mungu walishitakiwa kuwa “yeye mtaabishaji wa Israeli”. 1 Wafalme 18:17. Mji ukawekwa tena chini ya mkatazo, na Huss akarudishwa tena katika kijiji chake cha kuzaliwa. Akasema kuanzia mahali pa kubwa sana pa wazi, kwa jamii ya Wakristo wote, kabla ya kukata roho yake kama mshuhuda kwa ajili ya ukweli.TSHM 41.7

  Baraza kubwa likaitwa kukutana kule Constance (Udachi wa kusini na magharibi), likaitwa kwa mapenzi ya mfalme Sigismund na mmoja wapo wa mapapa wapinzani watatu, Yohana XXIII. Papa Yohana, ambaye tabia yake na maongozi yaliweza kufanya uchunguzi mbaya, hakusubutu kupinga mapenzi ya Sigismund. (Tazama Nyongezo). Makusudi makuu yaliyopashwa kutimizwa yalikuwa kuponya msukosuko katika kanisa kungoa mafundisho ya imani yasiyopatana na yale yaliyotangazwa na kanisa kuwa kweli. Wapinzani wawili hawa wa Papa wakaitwa kwenda mbele pamoja na John Huss. Wa kwanza walituma wajumbe wao. Papa John akaja na mashaka mengi, kuogopa kuhesabiwa kwa makosa ambayo yalileta haya kwa taji pia kwa ajili ya zambi zilizo ilinda. Huku alifanya kuingia kwake katika mji wa Constance na baridi kubwa, lililofanyiwa na mapadri na maandamano ya wafuasi wa mfalme. Juu ya kichwa chake chandarua cha zahabu, kuchukuliwa na waamuzi wane wakubwa. Mwenyeji (host) aliletwa mbele yake, na kupambwa kwa utajiri wa wakuu (cardinals) na watu wa cheo kikubwa vika urembo wakushangaza.TSHM 42.1

  Wakati ule ule msafiri mwengine alikuwa akikaribia Constance. Huss aliachana na rafiki zake kama kwamba hawataonana tena, kufikiri vile safari yake ilikuwa ikimwongoza kwa kingingi (mti wa kufungia watu wa kuchomwa moto). Alipata hati (ruhusa ya kupita) kwa mfalme wa Bohemia na hati ingine vile vile kwa mfalme Sigismund. Lakini alifanya matengenezo yake yote katika maoni yanayoweza kuelekea kifo chake.TSHM 42.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents