Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Juhudi kwa Ajili ya Masikilizano na Roma

  Frederic wa Saxony akaficha kwa uangalifu mawazo yake ya kweli kwa ajili ya Mtengenezaji. Kwa wakati ule akamlinda kwa uangalifu sana, kulinda mazunguko yake na yale ya maadui zake. Lakini wengi hawakujaribu kuficha huruma yao kwa Luther. “Chumba kidogo cha mwalimu,” akaandika Spalatin, “hakiwezi kuenea wageni wote waliojileta wenyewe kwa kumuzuru.” Hata wale wasiokuwa na imani katika mafundisho yake hawakuweza kujizuia lakini kushangalia ule ukamilifu uliomuongoza kuvumilia mauti kuliko kuvunja zamiri yake.TSHM 75.2

  Juhudi nyingi zikafanyika kwa kupata kuwezesha Luther kupatana na Roma. Wenye cheo na watawala wakamuonyesha kwamba kama akifanya hukumu yake pekee kupinga kanisa na baraza, hatahamishwa kukatiwa mbali ya ufalme na bila ulinzi. Tena akaombwa sana, kutii hukumu ya mfalme. Kwa hiyo hangaliogopa kitu. “Ninakubali,” akasema kwa kujibu, “na moyo wangu wote, kwamba mfalme, watawala, na hata Mkristo mnyonge sana, anapashwa kujaribu na kuhukumu kazi zangu; lakini kwa kanuni moja, kwamba wakamate neno la Mungu kuwa kipimo chao. Watu hawana kitu cha kufanya bali kukitii.”TSHM 75.3

  Kwa mwito mwengine akasema: “Ninakubali kukana cheti cha usalama wangu. Naweka nafsi yangu na maisha yangu katika mikono ya mfalme, lakini neno la Mungu--kamwe!” Akataja mapenzi yake kwa kutii baraza la watu wote, lakini kwa kanuni kwamba baraza itakiwe kuamua kufuatana na Maandiko. “Kwa ile inayohusu neno la Mungu na imani, kila Mkristo anakuwa muhukumu mwema kama Papa, ingawa anatetewa na milioni ya mabaraza.” Wote wawili rafiki na maadui, mwishowe, wakasadikishwa kwamba juhudi zaidi juu ya mapatano ingekuwa bure.TSHM 75.4

  Kama Mtengenezaji angelikubali jambo moja tu, Shetani na majeshi yake wangalipata ushindi. Lakini msimamo wake imara usiotikisika ulikuwa njia ya kuweka kanisa kwa uhuru. Mvuto wa mtu mmoja huyu aliyesubutu kufikiri na kutenda kwa ajili yake mwenyewe ulipashwa kwa kugeuza kanisa na ulimwengu, si kwa wakati wake mwenyewe tu, bali kwa vizazi vyote vya baadaye.TSHM 76.1

  Luther aliagizwa upesi na mfalme kurudi nyumbani mwake. Tangazo hili lingefuata kwa upesi na hukumu yake. Mawingu ya kutisha yakafunika njia yake, lakini kama alivyotoka Worms, moyo wake ukajaa na furaha na sifa.TSHM 76.2

  Baada ya kuondoka kwake, ili musimamo wake imara usizaniye kuwa uasi, Luther akaandika kwa mfalme: “Ninakuwa tayari kwa kutii kwa moyo kabisa kwa utukufu wako, katika heshima wala katika zarau, katika maisha ao katika mauti, na kuto kukubali kitu kingine cho chote isipokuwa Neno la Mungu ambalo mtu huishi kwa ajili yake. ... Wakati faida ya milele,inahusika mapenzi ya Mungu si mtu anapashwa kujiweka chini ya mtu. Kwani kujitoa kwa namna ile katika mambo ya kiroho ni kuabudu kwa kweli, na kunapaswa kutolewa kwa Muumba peke yake.”TSHM 76.3

  Kwa safari kutoka Worms, watawala wa kanisa wakakaribisha kama mfalme mtawa aliyetengwa kwa kanisa, na watawala wa serkali wakamheshimu mtu aliyelaumiwa na mfalme. Akalazimishwa kuhubiri, na bila kujali makatazo ya mfalme, akaingia tena kwa mimbara. “Siku ahidi kamwe mimi mwenyewe kufunga neno la Mungu kwa mnyororo,” akasema, “ama sitalifunga.”TSHM 76.4

  Mda kidogo baada ya kutoka Worms, wasimamizi wa Papa wakamshawishi mfalme kutoa amri juu yake. Luther alitangazwa kama “Shetani mwenyewe chini ya umbo la mtu anayevaa kanzu ya watawa.” Mara ruhusa yake ya kupita inapomalizika, mipango ilipaswa kukamatwa kwa ajili ya kukataza kumkaribisha, kumupa chakula wala kinywaji, ao kwa neno ao tendo, msaada wala kushirikiana naye. Alipashwa kutolewa mikononi mwa watawala, wafuasi wake pia kufungwa na mali yao kunyanganywa. Maandiko yake yalipashwa kuharibiwa, na mwishowe, wote wangesubutu kutenda kinyume cha agizo hili walihusika katika hukumu yake. Mchaguzi wa Saxe na watawala wote, waliokuwa rafiki sana wa Mtengenezaji, walipotoka Worms baada kidogo ya kutoka kwake, na agizo la mfalme likapokea ukubali wa baraza. Waroma walishangilia. Wakaamini mwicho wa Mtengenezaji kutiwa mhuri kabisa.TSHM 76.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents