Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kupiga Chapa Kulikatazwa

  Francis I akapendezwa kukusanya kwa uwanja wake watu wenye elimu ya maandiko kutoka kwa inchi zote. Lakini, wenye mafikara na juhudi ya kukomesha uzushi, baba huyu wa elimu akatoa amri kutangaza kwamba uchapaji wa vitabu umeondolewa pote katika Ufransa! Francis I ni mojawapo wa mifano ya historia kuonyesha kwamba akili ya masomo hailinde watu juu ya ushupavu wa dini na mateso.TSHM 104.4

  Wapadri wakadai kwamba aibu iliyofanyiwa Mbingu ya juu kwa hukumu ya misa isafishwe katika damu. Tarehe 21 Januari 1535, iliwekwa juu ya sherehe ya kutisha. Mbele ya kila mlango mwenge wa moto ukawashwa kwa ajili ya heshima ya “sakramenti takatifu.” Mbele ya usiku kucha makutano yakakutanika kwa jumba la mfalme.TSHM 105.1

  “Majeshi yakachukuliwa na askofu wa Paris chini ya chandaluwa nzuri, ... Baada ya majeshi kutembeza mfalme ... Francis I kwa siku ile hakuvaa taji, wala kanzu ya cheo.” Kwa kila mazabahu akainama kwa kujinyenyekea, si kwa ajili ya makosa iliyonajisi roho yake, ao damu isiyo na kosa iliyoharibu mikono yake, bali kwa ajili ya “zambi ya mauti” ya watu wake waliosubutu kuhukumu misa.TSHM 105.2

  Katika chumba kikubwa cha mjumba la askofu mfalme akatokea na katika maneno ya usemi wa hasira akasikitikia “makosa, matukano, siku ya huzuni na haya,” ambayo ilikuja juu ya taifa. Na akaalika waaminifu wake wa ufalme kusaidia kungoa baala ya “uzushi” ambayo ilitisha Ufransa kwa uharibifu. Machozi yakajaa kwa usemi wake, na mkutano wote ukaomboleza, kwa umoja wakasema kwa nguvu, “Tutaishi na kufa kwa ajili ya dini yaKikatoliki!”TSHM 105.3

  “Neema ile iletayo wokovu” ilionekana, lakini Ufransa ilipoangaziwa na mwangaza wake, ikautupilia mbali, ikachagua giza zaidi kuliko nuru. Wakaita ubaya wema, na wema ubaya, hata walipoanguka kuwa watu wa kuteswa kwa hila yao ya ukaidi. Nuru ambayo ingeweza kuwaokoa kwa udanganyifu, kwa kuchafua roho zao na kosa ya uuaji, wakaikataa kwa kuasi.TSHM 105.4

  Tena mkutano ukafanyika. “Kwa mwendo mfupi (majukwaa) mahali pa kunyongea watu yakajengwa mahali Wakristo wa Kiprotestanti walipashwa kuchomwa motoni wakiwa hai, na ilitengenezwa kwamba matata yawashwe wakati mfalme alipokaribia, na kwamba mwandamano ulipashwa kusimama kwa kushuhudia wauaji.” Hapakuwa na kutikisika kwa upande wa watu waliopashwa kufa. Kwa kushurutishwa kukana, mmoja akajibu: “Mimi naamini tu yale manabii na mitume waliyohubiri mbele na yale jamii lote la watakatifu waliamini. Imani yangu inakuwa na tumaini kwa Mungu ambaye atashinda mamlaka yote ya kuzimu.”TSHM 105.5

  Katika kufikia jumba la mfalme, makutano yakatawanyika na mfalme na maaskofu wakaondoka, walipokuwa wakishangilia wenyewe kwamba kazi ingeendelea kwa kutimiza maangamizo ya wapinga ibada ya dini.”TSHM 105.6

  Habari Njema ya amani ambayo Ufransa ilikataa ilipashwa kungolewa kweli, na matokeo yalikuwa ya kutisha. Tarehe 21 ya Januari 1793, mwandamano mwengine ukapita katika njia za Paris. “Tena mfalme alikuwa mwongozi mkuu; tena kukawa fujo na kulalamika; tena kukasikiwa kilio cha watu wengi walioteswa; tena kukawa majukwaa meusi; na matukio ya siku yakamalizika kwa mauaji na sana; Louis XVI, alipokuwa akishindana mikononi mwa walinzi wake wa gereza na wanyongaji, akakokotwa kwa gogo, na hapo akashikwa kwa nguvu nyingi hata shoka lilipoanguka, na kichwa chake kilichokatwa kikajifingirisha kwa jukwaa.” Karibu na mahali pale pale watu 2800 wakaangamizwa na machine yenye kisu cha kukata watu kichwa (guillotine). Matengenezo ikaonyesha kwa ulimwengu Biblia yenye kufunguliwa. Upendo usio na mwisho ukajulisha watu kanuni za mbinguni. Wakati Ufransa ilipokataa zawadi ya mbinguni, ikapanda mbegu ya uharibifu. Hakukuwa namna ya kuepuka matokeo yaliyotendeka ambayo mwisho ulikuwa mapinduzi na utawala wa kuhofisha.TSHM 106.1

  Farel shujaa na mwenye uhodari akalazimishwa kukimbia kutoka kwa inchi yake ya kuzaliwa na kwenda Uswisi. Lakini akaendelea kutumia mvuto uliokusudiwa juu ya matengenezo katika Ufransa. Pamoja na usaada wa watu wengine waliofukuzwa, maandiko ya Watengenezaji wa Ujeremani yakatafsiriwa katika Kifransa na pamoja na Biblia ya Kifransa ikachapwa kwa wingi sana. Kwa njia ya watu wa vitabu vya dini vitabu hivyo vikauzishwa kwa eneo kubwa sana katika Ufransa.TSHM 106.2

  Farel akaingia kwa kazi yake katika Uswisi kwa mwenendo mnyenyekevu wa mwalimu, akaingiza kwa werevu kweli za Biblia. Wengine wakaamini, lakini wapadri wakaja kusimamisha kazi, na watu wenye ibada ya sanamu wakaharakishwa kuipinga. “Hiyo haiwezi kuwa injili ya Kristo,” wapadri wakashurutisha, “kuona kuihubiri hakuwezi kuleta amani, bali vita.”TSHM 106.3

  Akaenda mji kwa mji, kuteseka na njaa, baridi, na kuchoka,na mahali pote katika ajali ya maisha yake. Akahubiri sokoni, ndani ya makanisa, mara zingine katika mimbara ya makanisa makubwa. Zaidi kuliko mara moja akapigwa karibu kufa. Lakini akaendelea mbele. Mwishowe akaona miji mikubwa na midogo iliokuwa ngome za kanisa la Katoliki yakafungua milango yao kwa injili.TSHM 106.4

  Farel alitamani kusimamisha bendera ya Waprotestanti katika Geneve. Kama mji huu ungaliweza kupatikana, ungalikuwa mahali pa kubwa kwa ajili ya Matengenezo katika Ufransa, Uswisi, na Italia. Miji mingi iliyokuwa kandokando ya miji midogo ikaamini.TSHM 106.5

  Pamoja na rafiki mmoja akaingia Geneve. Lakini akaruhusiwa kuhubiri mara mbili tu. Mapadri wakamwalika mbele ya baraza la kanisa, wakaja na silaha zilizofichwa chini ya makanzu yao, wakakusudia kutoa maisha yake. Inje ya chumba kulikuwa na watu wengi wenye hasira kuhakikisha kifo chake kama akiepuka baraza. Kuwako kwa waamzi na waaskari, ingawa hivyo wakamwokoa. Mapema sana asubuhi akapelekwa karibu ya ziwa mahali pa salama. Ndivyo ilivyokuwa mwisho wa juhudi yake ya kwanza ya kueneza injili huko Geneve.TSHM 107.1

  Kwa kusikilizwa mara ya pili, wakachagua chombo kizaifu sana; alikuwa kijana munyonge kwa sura hata akapokelewa bila furaha na marafiki wanaojidai kusimamia Matengenezo. Lakini mtu wa namna hii angeweza kufanya nini mahali Farel alikataliwa? “Mungu alichagua vitu zaifu vya dunia kupatisha vitu vya nguvu haya.” 1 Wakorinto 1:27.TSHM 107.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents