Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Shambulio la Mwisho la Kumpinga Mungu

  Shetani anashauriana pamoja na watu kuwa wakubwa. Wanatangaza ya kwamba jeshi ndani ya mji ni ndogo kwa kulinganisha na la kwao na linaweza kushindwa. Wafundi wa ujuzi wanafanya vyombo vya vita. Waongozi wa askari wanapanga watu wa vita katika makundi na sehemu.TSHM 324.1

  Mwishoni agizo la kuendelea mbele linatolewa, na jeshi lisilohesabika likaendelea, jeshi ambalo nguvu zenye kuunganika za vizazi vyote hazikuweza kamwe kuwa sawa. Shetani anakuwa mbele, wafalme na waaskari nao wanafuata. Kwa utaratibu wa kiaskari makundi katika mistari yakaendelea mbele ya uso wa dunia iliyovunjika hata kwa Mji wa Mungu. Kwa agizo la Yesu, milango ya Yerusalema Mpya ikafungwa, na majeshi ya Shetani yanajitayarisha kwa kushambulia.TSHM 324.2

  Sasa Kristo anatokea kutazama adui zake. Mbali juu ya mji, juu ya msingi wa zahabu yenye kungaa, ni kiti cha enzi. Juu ya kiti hiki cha enzi Mwana wa Mungu anakaa, na pembeni yake ni raia ya ufalme wake. Utukufu wa Baba wa Milele unamuzunguka Mwana wake. Kungaa kwa kuwako kwake kunatoka juu ya milango, kujaza dunia na mwangaza.TSHM 324.3

  Karibu sana na kiti cha enzi kunakuwa wale waliokuwa zamani na bidii katika kazi ya Shetani, lakini walipo ondoshwa kama vinga kutoka motoni, wakafuata Mwokozi wao kwa bidii sana. Wanaofuata ni wale waliokamilisha tabia katikati ya uwongo na uasi, walioheshimu sheria ya Mungu wakati walimwengu walipoitangaza kuwa iliondolewa, na mamilioni, wa vizazi vyote, waliouawa kama wafia dini kwa ajili ya imani yao. Mbali zaidi kunakuwa “makutano makubwa sana yasiyoweza mtu kuyahesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, ... wamevikwa mavazi myeupe, na matawi ya mitende katika mikono yao”. Ufunuo 7:9 . Vita yao imemalizika, ushindi wao umepatikana. Tawi la ngazi linafananisha shangwe, nguo yeupe ni alama ya haki ya Kristo ambayo saa imekuwa yao.TSHM 324.4

  Katika msongano wote ule pale hakuna watu wa kuhesabia wokovu kwao wenyewe kwa wema wao wenyewe. Hakuna kitu kinachosemwa cha kile walichoteseka nacho; sauti ya msingi ya kila wimbo wa sifa ni, Wokovu kwa Mungu wetu na kwa Mwana-Kondoo.TSHM 325.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents