Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Agano Jipya la Kifransa

    Lakini matumaini yao hayakutimia. Majaribu na mateso ikangoja wanafunzi wa Kristo. Walakini, wakati wa amani ukafika, ambao wangeweza kupata nguvu kwa kukutana na tufani, na matengenezo yakafanya maendeleo ya upesi. Lefévre akaanza kutafsiri wa Agano Jipya; na kwa wakati uleule ambapo Biblia ya Jeremani ya Luther ilipomalizika kutoka kwa mtambo wa kupigia chapa katika Wittenberg, Agano Jipya la Kinfransa likachapwa huko Meaux. Kwa upesi wakulima wa Meaux wakapata Maandiko matakatifu. Watu wa kazi katika mashamba, wafundi katika kiwanda cha kufanyia kazi, wakafurahishwa na kazi yao ya kila siku kwa kuzungumza habari ya damani ya kweli ya Biblia. Ijapo walikuwa watu wa cheo cha chini kabisa, bila elimu na kazi ngumu ya ukulima, matengenezo, uwezo unaogeuza, wa neema ya Mungu ukaonekana katika maisha yao.TSHM 98.4

    Nuru iliyoangaza huko Meaux ikatoa nyali yake mbali. Kila siku hesabu ya waliogeuka ilikuwa ikiongezeka. Hasira kali ya serkali ya kanisa ikakomeshwa kwa mda kwa kizuio cha mfalme, lakini wafuasi wa Papa wakashinda mwishowe. Mti wakuchoma wa pinga dini kukawashwa. Wengi walioshuhudia juu ya ukweli wakawa katika miako ya moto.TSHM 99.1

    Ndani ya vyumba vikubwa vya majumba na majumba ya kifalme, kulikuwa roho za kifalme ambamo ukweli ulikuwa wa damani kuliko utajiri ao cheo ao hata maisha. Louis de Berquin alikuwa mzaliwa wa jamaa ya cheo kikubwa, aliyejitoa kwa majifunzo, mwenye kuadibishwa na tabia isiyolaumiwa. “Akakamilisha kila namna ya wema kwa kushika mafundisho ya Luther katika machukio makuu ya kipekee.” Lakini, kwa bahati njema akaongozwa kwa Biblia, akashangazwa kupata pale “si mafundisho ya Roma, bali mafundisho ya Luther.” Akajitoa mwenyewe kwa kazi ya injili.TSHM 99.2

    Mamlaka ya Papa ya Ufransa ikamtia gerezani kama mpinga imani ya dini, lakini akafunguliwa na mfalme. Kwa miaka nyingi Francis alikuwa akisitasita kati ya Roma na Matengenezo. Mara tatu Berquin akafungwa na mamlaka ya Papa, na akafunguliwa na mfalme, aliyekataa kumtoa kafara kwa ukorofi wa serkali ya kanisa. Berquin akazidi kuonywa juu ya hatari iliyotaka kumpata katika Ufransa na akalazimishwa kufuata hatua za wale waliokwenda kutafuta usalama katika kuhamishwa kwa mapenzi mbali na kwao.TSHM 99.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents