Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Maonyo Yalitimilika

  Kwa wakati kabisa uliotajwa, Turkey ilikubali ulinzi wa mamlaka za mapatano ya Ulaya na kwa hivyo ikajitia yenyewe chini ya utawala wa mataifa ya Kikristo. Jambo kwa halisi kweli likatimiliza ukashiri. (Tazama Nyongezo.) Watu wengi walisadikishwa na kanuni za maelezo ya unabii yaliyokubaliwa na Miller na wafuasi wake. Watu wenye elimu na cheo wakajiunga pamoja na Miller katika kuhubiri na kutangaza maonyo yake. Tangu 1840 hata 1844 kazi ikaenea kwa upesi.TSHM 159.5

  William Miller alikuwa na akili za kichwa cha nguvu, na akaongeza kwa haya hekima ya mbinguni kwa kujiunga mwenyewe na Chemchemi ya hekima. Aliamuru heshima po pote, ukamilifu na tabia njema vilitumiwa. Kwa damani unyenyekevu wa Kikristo, alikuwa muangalifu na mpole kwa wote, tayari kusikiliza wengine na kupima mabishano yao. Alijaribu maelezo yote kwa Neno la Mungu, na mawazo yake halisi na maarifa ya Maandiko vikamwezesha kukanusha makosa.TSHM 160.1

  Lakini, kama pamoja na Watengenezaji wa kwanza, kweli alizoonyesha hazikukubaliwa na walimu wengi wa dini. Kwa hivyo hawa hawakuweza kudumisha hali yao kwa Maandiko, wakarejea kwa mafundisho ya watu, haya kiasili cha Wababa. Lakini Neno la Mungu lilikuwa ni ushuhuda pekee uliokubaliwa na wahubiri wa kweli wa kuja kwa Yesu. Cheko na zarau vilitumiwa kwa upande wa adui katika kusingizia wale waliotazamia kwa furaha juu ya kurudi kwa Bwana wao na walikuwa wakijitahidi kuishi maisha takatifu na kutayarisha wengine kwa kuonekana kwake. Ilifanyika kuonyesha zambi kwa kujifunza mambo ya unabii wa kuja kwa Kristo na mwisho wa dunia. Kwa hivyo kazi ya mapadri wa watu wengi ikapunguza imani katika Neno la Mungu. Mafundisho yao yakafanya watu kuwa watu kutokuwa Waaminifu, na wengi wakajiruhusu kwa kutembea kwa tamaa mbaya. Halafu watenda maovu wakayaweka yote juu ya Waadventisti.TSHM 160.2

  Ingawa Miller akavuta makundi ya wasikilizi wenye akili, jina lake lilitajwa kwa shida na magazeti ya dini isipokuwa tu kwa cheko ao mashitaki. Waovu, waliposukumwa na walimu wa dini, wakakimbilia kwa mabisho ya matukano juu yake na kazi yake. Mzee huyu mwenye imvi aliyeacha makao yake ya kupendeza kwa kusafiri kwa garama yake mwenyewe kuletea dunia onyo kubwa la hukumu inayokaribia akasitakiwa kama upumbavu.TSHM 160.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents