Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  “Nyota Zitaanguka”

  Katika mwaka 1833 ishara za mwisho zikaonekana zilizoahidiwa na Mwokozi kama dalili ya kuja kwake kwa mara ya pili: “Nyota zitaanguka toka mbinguni.” Na Yoane katika Ufunuo akasema, “Na nyota za mbinguni zikaanguka juu ya dunia kama vile mtini unavyotupa matunda mabichi yake, wakati unapotikiswa na upepo mkubwa.” Matayo 24:29; Ufunuo 6:13. Unabii huu ulipata utimilifu wa kushangaza katika wingi wa vimondo (nyota ipitayo upesi mbinguni) vya Novemba 13, 1833, ni tamasha ya kushangaza ya nyota ambayo historia hulinda kumbukumbu yake. “Kamwe mvua haikuanguka tena kubwa kuliko vimondo vilivyoanguka juu ya dunia; mashariki, mangaribi, kaskazini na kusini, ilikuwa namna moja. Katika neno moja, mbinguni pote kulionekana katika mwendo... Tangu saa nane hata asubui, mbingu kuwa bila mawingu kabisa na kweupe, mwendo wa daima wa miangaza yenye kungaa ya ajabu ikalindwa mbinguni mwote.”TSHM 158.3

  Ilionekana kwamba nyota zote za mbinguni zilipatana kukutana pahali pa karibu pa opeo, na zilikuwa zikiendelea kurushwa wakati ule ule, kwa upesi wa umeme, kwa pande zote za upeo wa macho; na huku hazikuisha--maelfu kwa upesi katika njia za maelfu, kama kwamba ziliumbwa kwa ajili ya tukio lile.” “Picha halisi zaidi ya mtini kuangusha tini zake zinapopeperushwa na upepo wa nguvu, ndiyo si vyepesi kueleza tukio hili.”TSHM 159.1

  Katika gazeti la biashara la New York la tarehe 14, Novemba 1833, kukatokea nakala kwa ajili ya jambo hili; “Hakuna mtu wa elimu ya elimu zote (philosophe) wala mwalimu aliyetoa habari wala kuandika tukio, ninawaza, kama lile la jana asubui. Nabii miaka elfu moja mia nane iliyopita akaitabiri sawasawa, kama tukiwa kwa hatari ya kufahamu kwamba kuanguka kwa nyota hakika ni kuanguka kwa nyota,... katika maana ya pekee kwamba inawezekana kwa kweli.”TSHM 159.2

  Ndivyo ilivyokuwa onyesho la dalili zile za kuja kwake, kuhusu habari ambazo Yesu aliambia wanafunzi wake: “Wakati munapoona maneno haya yote, mjue ya kuwa yeye ni karibu, hata kwa milango.” Matayo 24:33. Wengi walioshuhudia kuanguka kwa nyota walikutazama kama mjumbe wa hukumu ijayo.TSHM 159.3

  Katika mwaka 1840 utimilizo kubwa mwingine wa unabii ukaamsha usikizi wa mahali pengi. Miaka miwili mbele, Josiah Litch akatangaza habari ya Ufunuo 9, kutabiri kuanguka kwa Ufalme wa Ottoman “Katika A.D. 1840, siku moja katika mwezi wa Agosti.” Siku chache tu mbele ya kutimilika kwake akaandika: “Itamalizika kwa tarehe 11 ya Agosti, 1840, wakati mamlaka ya Ottoman katika Constantinople kuweza kutazamiwa kuvunjika.”TSHM 159.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents