Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ushindi wa Upendo wa Mungu

    Huko upendo na huruma ambavyo Mungu mwenyewe alivyopanda katika roho yatapata mazoezi ya kweli na mazuri kabisa. Umoja ulio safi pamoja na viumbe vitakatifu na waaminifu wa vizazi vyote, vifungo takatifu vinavyofunga pamoja “jamaa lote mbinguni na duniani”--hivi vinasaidia kuanzisha furaha ya waliokombolewa. Waefeso 3:15.TSHM 331.1

    Huko, akili ya kuishi milele zitatazama sana na furaha ya milele maajabu ya uwezo wa uumbaji, siri za upendo wa ukombozi. Kila akili itakuzwa, kila uwezo wa kufahamu utaongezwa. Upataji wa maarifa hautaondoa utendaji. Mambo makubwa sana yataendeshwa mbele, tamaa za juu sana zitafikiwa, tamaa za nguvu zitatimilika. Na tena hapo kutatokea vimo vipya vya kushinda, maajabu mapya ya kushangaa, kweli mpya ya kufahamu, makusudi mapya ya kuita nguvu za akili na roho na mwili.TSHM 331.2

    Mali yote ya ulimwengu itafunguliwa kwa waliokombolewa wa Mungu. Wanapofunguliwa kwa mauti, wataruka bila kuchoka kwa dunia za mbali. Watoto wa dunia wataingia katika furaha na hekima ya viumbe vile havikuanguka na kugawanya hazina za maarifa yaliyopatikana kupitia vizazi kwa vizazi. Pamoja na ndoto isiyo na giza watatazama kwa utukufu wa uumbaji--jua na nyota na mambo yote, yote katika utaratibu wao ulioagizwa kuzunguka kiti cha enzi cha Mungu.TSHM 331.3

    Na miaka ya milele, kama inavyopita upesi, italeta daima na zaidi mambo ya funuo tukufu ya Mungu na ya Kristo. Watu watakavyojifunza zaidi habari ya Mungu, ndivyo zaidi watakayoshangaa juu ya tabia yake. Kwa namna Yesu atakavyofunua mbele yao utajiri wa ukombozi na kazi bora za kushangaza katika mashindano makubwa na Shetani, mioyo ya waliokombolewa wanafurahi sana na kufanya ibada, na sauti elfu kumi mara elfu kumi zinaungana kuongeza nguvu la itikio la wimbo wa sifa.TSHM 331.4

    “Na kila kiumbe kilicho mbinguni na juu ya dunia na chini ya dunia na vile ndani ya bahari, na vyote vilivyo ndani yake, nilivisikia, vikisema: Baraka na heshima na utukufu na uwezo kwa yeye anayeketi juu ya kiti cha enzi, na kwa Mwana-Kondoo hata milele na milele”. Ufunuo 5:13.TSHM 331.5

    Vita kuu imekoma. Zambi na wenye zambi hawako tena. Ulimwengu wote mzima ni safi. Kwa Yeye aliyeumba vyote, kunajaa uzima na nuru na furaha po pote katika ufalme za anga pasipo mpaka. Kutoka kwa chembe ndogo hata kwa ulimwengu mkubwa sana, vitu vyote, vyenye uhai na vitu visivyokuwa na uhai, katika uzuri wao pasipo kivuli na furaha kamili, vitatangaza ya kwamba Mungu ni upendo.TSHM 331.6

    *****

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents