Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mvumbuzi Hodari wa Kosa

  Wycliffe alikuwa mvumbuzi hodari wa kosa na akapambana bila woga juu ya matumizi mabaya yaliyoruhusiwa na Roma. Alipokuwa padri wa mfalme, akawa shujaa kwa kukataa malipo ya kodi yaliyodaiwa na Papa kutoka kwa mfalme wa Uingereza. Majivuno ya Papa ya mamlaka juu ya watawala wa ulimwengu yalikuwa kinyume kwa vyote viwili kweli na ufunuo. Matakwa ya Papa yalichochea hasira, na mafundisho ya Wycliffe yalivuta akili za uongozi wa taifa. Mfalme na wakuu walikusanyika kwa kukataa malipo ya kodi.TSHM 31.1

  Watu waliojitenga na mambo ya dunia, maskini wakajaa katika Uingereza, kumwanga sumu juu ya ukubwa na kufanikiwa kwa taifa. Maisha ya watawa (moines) ya uvivu na uombaji wa vitu ao mali haikuwa tu gharama kubwa juu ya mali ya watu, wageuza kazi nzuri kuwa ya kuzarauliwa. Vijana walipotoka na kuharibika. Wengi walishawishwi kujitoa wao wenyewe kwa maisha ya watawa si kwa kukosa ukubali wa wazazi tu, bali bila ufahamu wao na kinyume cha mwito wao. Kwa “chukizo hili lisilo la kibinadamu” kama vile Luther baadaye alilitia “kuonyesha dalili ya mbwa mwitu zaidi na mjeuri kuliko ya Mkristo na mtu, “ilivyokuwa” mioyo ya watoto ikiwa migumujuu ya wazazi wao.TSHM 31.2

  Hata wanafunzi katika vyuo vikubwa (universites) walidanganywa na watawa na kuvutwa kwa kuungana namaagizo yao. Mara waliponaswa katika mtego ilikuwa haiwezekani kupata uhuru. Wazazi wengi walikataa kutuma vijana wao katika vyuo vikubwa. Vyuo vikazoofika, na ukosefu wa elimu ukaenea pote.TSHM 31.3

  Papa akatoa kwa watawa hawa uwezo kwa kusikia maungamo na kutoa rehema-shina la uovu mkubwa. Wakageuka kwa kuzidisha faida zao, watu waliojitenga kwa mambo ya kidunia walikuwa tayari kabisa kutoa masamaha hata wavunja sheria walikuwa wakienda mara kwa mara kwao, na makosa mabaya zaidi yakaongezeka kwa haraka. Zawadi zilizopasa kusaidia wagonjwa na maskini zikaenda kwa watawa. Utajiri wa watu waliojitenga kwa mambo ya kidunia ukaongezeka daima, na majumba yao makubwa na meza za anasa vikaonyesha zaidi kuongezeka kwa umaskini kwa taifa. Huku watawa wakaendelea kukaza uwezo wao juu yawengi waliokuwa katika imani ya uchawi na wakawaongoza kuamini kuwa kazi yote ya dini iliyoonyesha ukubali wa mamlaka ya Papa, kusujudu watakatifu, kufanya zawadi kwa watawa, hili lilikuwa la kutosha kwa kujipatia nafasi mbinguni!TSHM 31.4

  Wycliffe kwa maarifa safi, akashambulia mizizi ya uovu, kutangaza kwamba utaratibu wenyewe ni wa uongo na ulipaswa kuondolewa kabisa. Mabishano na maswali yalikuwa yakiamshwa. Wengi walikuwa wakiongozwa kujiuliza kwamba hawakupaswa kutafuta rehema zao kwa Mungu zaidi kuliko kwa askofu wa Roma. (Tazama Nyongezo). “Watawa na mapadri wa Roma,” wakasema, “wako wanatula kama ugonjwa unaoitwa (cancer), Mungu anapashwa kutuokoa, kama sivyo watu wataangamia”. Watawa waombezi waliojidai kwamba walikuwa wakifuata mfano wa Mwokozi, kutangaza kwamba Yesu na wanafunzi wake walikuwa wakisaidiwa kwa ajili wema wa watu. Madai haya yakaongoza watu wengi kwa Biblia kujifunza ukweli wao wenyewe.TSHM 32.1

  Wycliffe akaanza kuandika na kuchapa vimakaratasi na tuvitabu juu ya watawa, kuita watu kwa mafundisho ya Biblia na Muumba wake. Si kwa njia ingine bora kuliko angeweza kutumia kwa kumuangusha yule mnyama mkubwa ambaye Papa alimufanyiza, na ndani yake mamilioni waliokamatwa watumwa.TSHM 32.2

  Wycliffe alipoitwa kwa kutetea haki za ufalme wa Uingereza juu ya kujiingiza kwa Roma, alitajwa kuwa balozi wa kifalme katika inchi ya Hollandi. Hapo ilimfanya rahisi kupelekeana habari na mapadri kutoka Ufaransa, Italia, na Ispania, na alikuwa na bahati ya kutazama nyuma matukio yaliyofichwa kwake huko Uingereza. Katika wajumbe hawa kutoka kwa baraza ya hukumu ya Papa akasoma tabia ya kweli ya serekali ya kanisa. Akarudi Uingereza kukariri mafundisho yake ya kwanza na juhudi kubwa, kutangaza kuwa kiburi na udanganyifu vilikuwa miungu ya Roma.TSHM 32.3

  Baada ya kurudi Uingereza, Wycliffe akapokea kutoka kwa mfalme kutajwa kuwa kasisi ya Lutterworth. Jambo hili lilikuwa uhakikisho kwamba mfalme alikuwa bado hajachukiwa na kusema kwake kwa wazi. Muvuto wa Wycliffe ukaonekana katika muundo wa imani ya taifa.TSHM 32.4

  Radi za Papa zikatupwa upesi juu yake. Matangazo matatu ya Papa yakatumwa kuamuru mipango ya gafula ya kunyamazisha mwalimu wa “upinzani wa mafundisho ya dini”TSHM 32.5

  Kufika kwa matangazo ya Papa kukawekwa agizo katika Uingereza pote kufungwa kwa mpinga wa dini. (Tazama Nyongezo). Ilionekana kweli kwamba Wycliffe alipashwa kuanguka upesi kwa kisasi cha Roma. Lakini yeye aliyetangaza kwa mmojawapo wa zamani, “usiogope ...: mimi ni ngabo yako” (Mwanzo 15:1), akanyosha mkono wake kulinda mtumishi wake. Kifo kikaja, si kwa Mtengenezaji, lakini kwa askofu aliyeamuru uharibifu wake.TSHM 32.6

  Kifo cha Gregoire XI kulifuatwa na uchaguzi wa mapapa wawili wapinzani. (Tazama Nyongezo). Kila mmoja akaita waaminifu wake kufanya vita kwa mwengine, kukaza maagizo yake ya hofu kuu juu ya wapinzani wake na ahadi za zawadi mbinguni kwa wafuasi wake. Makundi ya wapinzani yalifanya yote yaliweza kufanya mashambuliano mmoja kwa mwengine, na Wycliffe kwa wakati ule alikuwaakipumzika.TSHM 33.1

  Mutengano pamoja na bishano yote na uchafu ambayo vilitayarisha njia kwa Mategenezo kwa kuwezesha watu kuona hakika hali ya kanisa la Roma. Wycliffe akaita watu kuzania kama mapapa hawa wawili hawakuwa wakisemea ukweli katika kuhukumiana mmoja kwa mwengine kama mpinga Kristo.TSHM 33.2

  Akakusudia kwamba nuru inapaswa kuenezwa kila pahali katika Uingereza, Wycliffe akatengeneza kundi la wahubiri, kujishusha, watu waliojitoa waliopenda ukweli na kuamania kuipanua. Watu hawa walikuwa wakifundisha katika barabara za miji mikubwa,na katika njia inchini, wakitafuta wazee, wagonjwa, na maskini, na wakawafungulia habari za furaha za neema ya Mungu.TSHM 33.3

  Kule Oxford, Wycliffe akahubiri Neno la Mungu ndani ya vyumba vikubwa vya chuo kikuu. Akapata cheo cha Daktari (Docteur) wa injili. Lakini kazi kubwa mno ya maisha yake ilikuwa kutafsiri kwa Maandiko katika lugha ya Kiingereza, ili kila mtu katika Uingereza aweze kusoma kazi za ajabu za Mungu.TSHM 33.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents