Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Namna Mafundisho ya Uongo Yaliingia

  Mojawapo miongoni mwa makosa haya makubwa ya wazi ni imani ya kutokufa kwa roho ya mtu na ufahamu wa nafsi katika mauti. Mafundisho haya yaliweka msingi ambao Roma ikaanzisha sala kwa watakatifu na ibada ya Bikira Maria. Kutokana na hiyo, uzushi juu ya mateso ya milele kwa ajili ya mtu asiyetubu, ambayo yaliingizwa mwanzoni katika imani ya Papa.TSHM 19.2

  Ndipo njia ikatengenezwa kwa kuingiza uvumbuzi mwingine wa kipagani, ambao Roma iliita “toharani”, na iliotumiwa kwa kuogopesha makundi ya wajinga na ya kuamini mambo ya uchawi. Usishi huu uliamini kuwako kwa pahali pa mateso ambapo roho zisizostahili hukumu ya milele, zinapaswa kuteseka juu ya malipizi ya zambi zao, na kutoka pale, zikiisha takaswa, zinakubaliwa mbinguni (Tazama Nyongezo).TSHM 19.3

  Uvumbuzi mwingine ukahitajiwa, kuwezesha Roma kupata faida kwa njia ya woga na makosa ya wafuasi wake. Huu ulitolewa na mafundishojuu ya ununuzi wa huruma (indulgences). Ondoleo nzima la zambi za sasa, zilizopita na za wakati ujao liliahidiwa kwa wale waliojitoa kwa vita vilivyofanywa na Papa kwa ajili ya kupanua mamlaka yake, kwa kulipiza adui zake ao kuangamiza wale waliosubutu kukataa mamlaka yake ya kiroho. Kwa njia ya kulipa mali katika kanisa wanaweza kujiokoa katika zambi zao, na pia kuokoa roho za rafiki zao zinazoteseka katika miako ya moto. Kwa njia hiyo Roma ikajaza masanduku makubwa yake na kusaidia fahari yake, anasa na uovu wa kujidai kuwa wajumbe wa Yule asiyekuwa na pahali pa kuweka kichwa chake (Tazama Nyongezo).TSHM 19.4

  Meza ya Bwana likapigwa na kafara ya ibada ya sanamu ya misa. Mapadri wa Papa wakajidai kufanya mkate na divai vya Meza ya Bwana kuwa mwili wa kweli na damu ya kweli ya Bwana Yesu Kristo”. Kwa majivuno ya kutukana Mungu, kwa wazi wakadai uwezo wa kuumba Mungu, Muumba wa vitu vyote. Wakristo wakalazimishwa maumivu ya kifo, kuungama imani yao katika uzushi wa machukizo ya kutukana mbingu.TSHM 19.5

  Katika karne ya kumi na tatu kile chombo kikali sana kati ya vyombo vya Papa kikaanzishwa-Baraza kuu la kuhukumia wazushi wa dini (Inquisition). Katika mabaraza yao ya siri Shetani na malaika zake walitawala roho za watu waovu. Bila kuonekana katikati Malaika wa Mungu alisimama, alipoandika kwa uaminifu ukumbusho wa maagizo yao maovu ya kutisha na kuandika historia ya matendo yao mabaya sana kuonekana machoni pa watu. “Babeli Mkuu” “analewa kwa damu ya watakatifu”. Tazama Ufunuo 17:5,6. Miili iliyoteseka ya mamilioni ya wafia dini (martyrs) ikalalamika mbele ya Mungu kwa ajili ya kisasi juu ya ule uwezo wa mkufuru.TSHM 20.1

  Papa akawa mtawala mkali peke yake wa dunia yote. Wafalme na wafalme wakubwa (empereurs) walitii maagizo ya askofu wa Roma. Kwa muda wa mamia ya miaka mafundisho ya Roma yakakubaliwa na wengi. Waongozi wake wakaheshimiwa na kusaidiwa sana. Kamwe tangu wakati ule, kanisa la Roma lilikuwa halijafikia kadiri ya cheo kikubwa, cha fahari, ao uwezo wa namna ile.TSHM 20.2

  Lakini “azuhuri ya cheo cha Papa ilikuwa usiku wa manane wa wanadamu”.TSHM 20.3

  Maandiko matakatifu yalikuwa karibu bila kujulikana. Waongozi wa kanisa la Roma walichukia nuru iliyofunua zambi zao. Sheria ya Mungu, kipimo cha haki, ilipoondolewa, wakatumia uwezo bila kizuio. Majumba makubwa ya Papa na maaskofu yalikuwa monyesho ya upotovu wa machukizo. Maaskofu wengine walikuwa na makosa ya maovu sana hata wakajaribu kuwaondosha kama wanyama wa kutisha wasioweza kuvumiliwa. Kwa muda wa karne nyingi Ulaya haikufanya maendeleo kamwe katika maarifa ya kweli, mambo ya ufundi na maendeleo ya jamii. Ukristo ukapatwa na kupooza kwa tabia na maarifa... Ndiyo yalikuwa matokeo ya kufukuza Neno la Mungu!TSHM 20.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents