Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mnyama wa Pembe Mbili Mfano wa Mwana-Kondoo

    Unabii wa Ufunuo 13 unatangaza ya kwamba mnyama wa pembe mbili mfano wa mwana-kondoo atafanya “dunia na wanaokaa ndani yake” kuabudu kanisa la Rome--lililofananishwa na mnyama “alikuwa mfano wa chui. “Mnyama wa pembe mbili itasema vilevile “wale wanaokaa juu ya dunia, kufanyia sanamu yule mnyama”. Tena, naye anawafanya wote, “wadogo na wakubwa, na matajiri na maskini na wahuru na wafungwa,” wapokee chapa cha mnyama. Ufunuo 13:11-16. Amerika ni uwezo uliofananishwa na nyama yule wa pembe mbili mfano wa mwana-kondoo. Unabii huu utatimilika wakati Mwungano wa mataifa ya Amerika watakapokaza kushika siku ya kwanza (dimanche), ambayo Roma inadai kama hakikisho kwa mamlaka yake.TSHM 282.1

    “Nikaona kimoja cha vichwa vyake, kama kimetiwa kidonda cha kufa; kidonda chake cha kufa kikapona; dunia yote ikastaajabia mnyama yule”. Ufunio 13:3. Kidonda cha kufa kinaonyesha kuanguka kwa kanisa la Roma (Papa) katika mwaka 1798. Baada ya hii, asema nabii, “kidonda chake cha kufa kikapona: na dunia yote ikastaajabia nyama yule”. Paulo akataja ya kwamba “mwana wa uharibifu” ataendelea na kazi yake ya madanganyo kwa mwisho kabisa wa wakati”. 2 Tesalonika 2:3-8. Na “watu wote wanaokaa juu ya dunia watamwabudu, wale, majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima”. Ufunuo 13:8. Katika Ulimwengu wa Zamani na mpya, kanisa la Papa litapokea heshima kwa heshima iliyotolewa kwa siku ya kwanza (dimanche).TSHM 282.2

    Tangu katikati ya karne ya kumi na tisa, wanafunzi wa unabii wameonyesha ushuhuda huu kwa ulimwengu. Sasa tunaona maendeleo ya upesi kwa utimilifu wa unabii. Kwa waalimu wa Waprotestanti kunakuwa na madai ya namna moja ya mamlaka ya Mungu kwa ajili ya kushika siku ya kwanza (dimanche), na ukosefu wa namna moja wa ushuhuda wa maandiko, kama kwa waongozi wa kanisa la Roma (Papa). Tangazo ya kwamba hukumu za Mungu zinafikia watu kwa ajili ya kuvunja sabato ya siku ya kwanza (di-manche) litarudiliwa: tayari linaanza kulazimishwa.TSHM 282.3

    Ni ajabu kwa werevu, Kanisa la Roma. Linaweza kusoma kitu gani kinapaswa kuwa--ya kwamba makanisa ya Waprotestanti yanatoa heshima yake kwa Roma wanapokubali sabato ya uwongo na ya kwamba wanajitayarisha kuikaza kwa namna kanisa lenyewe lilifanya katika siku zilizopita. Kwa upesi gani litapata usaada wa Waprotestanti katika kazi hii si vigumu kuelewa.TSHM 282.4

    Kanisa la Wakatoliki wa Roma linafanya muungano mkubwa chini ya mamlaka ya Papa, mamilioni ya washiriki wake katika kila inchi wanaagizwa utii kwa Papa, hata taifa lao liwe la namna gani wala serkali yao. Ijapo wanaweza kuapa kiapo kuahidi uaminifu kwa serikali, lakini kinyume cha hii kunakuwa kiapo wala naziri ya uaminifu kwa Roma.TSHM 283.1

    Historia inashuhudia juu ya nguvu ya uerevu wa Roma kujiingiza mwenyewe katika mambo ya mataifa, kuweza kupata ustawi, kuendesha makusudi yake mwenyewe, hata kwa maangamizi ya watawala na watu.TSHM 283.2

    Ni majivuno ya Roma kwamba hawezi kubadili kamwe. Waprotestanti hawajui wanalolifanya wanapokusudia kukubali usaada wa Roma kwa kazi ya kutukuza siku ya kwanza (dimanche). Kwa namna wanavyoelekea kwa kusudi lao, Roma inakusudia kuimarisha mamlaka yake, kujipatia tena uwezo wake uliopotea. Acha kanuni kwanza liimarishwe na kanisa liweze kutawala uwezo wa serikali; na desturi za dini ziweze kukazwa na sheria za dunia; kwa kifupi, ya kwamba mamlaka ya kanisa na ya serikali itatawala zamirina ushindi wa Roma umehakikishwa.TSHM 283.3

    Jamii ya Waprotestanti itajifunza namna gani makusudi ya Roma inavyokuwa, ila tu wakati unapokwisha kupita kwa kuepuka mtego. Linasitawi kwa utulivu katika mamlaka. Mafundisho yake yanatumia mvuto katika vyumba vya sheria, katika makanisa, na katika mioyo ya watu. Linaimarisha nguvu zake kuendesha maangamizo yake wakati mda utakapofika kwa kushangaza. Yote linayotumaini (kanisa) ni mahali pafaapo. Ye yote atakayeamini na kutii Neno la Mungu atapata laumu na mateso.TSHM 283.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents