Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Luther Anashitakiwa kuwa Mpinga Imani ya Dini

    Kwa kujifunza na usemaji unaokolea, Aleander akajitahidi mwenyewe kuangusha Luther kama adui wa kanisa na serekali. “Haki,, makosa ya Luther yametosha”, akatangaza kwa kushuhudia kuchomwa kwa mamia elfu wapinga imani ya dini.”TSHM 66.1

    “Ni wanani watu hawa wote wa Luther? Kundi la waalimu wenye kiburi, mapadri waovu, watawa wapotovu, wanasheria wajinga, na wenye cheo walioaibishwa. ...Kundi la katoloki si linawapita mbali sana kwa wingi, kwa akili na kwa uwezo! Amri ya shauri moja la kusanyiko hili tukufu litaangazia wanyenyekevu, litaonya wasio na busara, litaamua wenye mashaka na kuimarisha wazaifu.”TSHM 66.2

    Mabishano ya namna ile ile ingali inatumiwa juu ya wote wanaosubutu kutoa mafundisho kamili ya Neno la Mungu. “Ni wanani hawa wahubiri wa mafundisho mapya? Wanakuwa si wenye elimu, wachache kwa hesabu, na wa cheo cha maskini sana. Lakini wakijidai kuwa na ukweli, na kuwa watu waliochaguliwa na Mungu. Wanakuwa wajinga na waliodanganyiwa. Namna gani kanisa letu ni kubwa sana kwa hesabu na mvuto!” Mabishano haya hayako na nguvu zaidi sasa kuliko siku za Mtengenezaji.TSHM 66.3

    Luther hakuwa pale, pamoja na maneno ya kweli wazi wazi na ya kusadikisha ya Neno la Mungu, kwa kushinda shujaa Papa. Watu karibu wote walikuwa tayari, si kwa kumuhukumu tu, yeye na mafundisho yake, bali, ikiwezekana, kuongoa upinzani wa imani ya dini. Yote Roma iliweza kusema katika kujitetea mwenyewe imesemwa. Lakini tofauti kati ya ukweli na uwongo ingeonekana wazi zaidi namna wangeweza kujitoa wazi wazi kwa vita.TSHM 66.4

    Sasa Bwana akagusa moyo wa mshiriki mmoja wa baraza atoe maelezo ya matendo ya jeuri ya Papa. Duc Georges wa Saxe akasimama katika mkutano huu wa kifalme; na akaonyesha sawasawa kabisa uwongo na machukizo ya kanisa la Roma:TSHM 66.5

    “Kuzulumu ... kunapaza sauti juu ya Roma. Haya yote imewekwa kando na shabaha yao moja tu ni ... pesa, pesa, pesa, ... ili wahubiri wanaopashwa kufundisha ukweli, wasinene kitu kingine isipokuwa uongo, na si kuwavumilia tu, lakini kuwalipa, kwani namna wanazidi kusema uongo, ndipo wanazidi kupata faida. Ni kwa kisima hiki kichafu maji haya machafu hutiririka. Mambo ya washerati na ulevi. Hunyoosha mkono kwa uchoyo ... Ole! ni aibu iliyoletwa na askofu kinachotupa roho maskini nyingi katika hukumu ya milele. Matengenezo ya mambo yote inapaswa kufanyika.” Sababu mnenaji alikuwa adui maalumu wa Mtengenezaji alitoa mvuto mkubwa kwa maneno yake.TSHM 66.6

    Malaika wa Mungu wakatoa nyali za nuru katika giza ya uovu na ikafungua mioyo kwa ukweli. Uwezo wa Mungu wa ukweli ukatawala hata maadui wa Matengenezo na ukatayarisha njia kwa kazi kubwa ambayo ilikaribia kutimizwa. Sauti ya Mmoja mkuu kuliko Luther ikasikiwa katika mkutano ule.TSHM 67.1

    Baraza ikawekwa kwa kutayarisha hesabu ya mambo yote yaliyo kuwa magandamizo ambayo yalikuwa mazito kwa watu wa Ujeremani. Oroza hii ikaonyeshwa kwa mfalme, na kumuomba achukue hatua kwa kusahihisha mambo mabaya haya. Wakasema waombaji, “Ni wajibu wetu kuzuia maangamizi na aibu ya watu wetu. Kwa sababu hiyo sisi wote pamoja tunakuomba kwa unyenyekevu sana, lakini kwa namna ya haraka sana, kuagiza matengenezo ya mambo yote na kufanya itimilike.”TSHM 67.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents