Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kufunga Kazi ndani ya Pahali patakatifu

  Katika mfano wa Matayo 22 hukumu inafanyika mbele ya arusi. Mbele ya arusi mfalme anaingia kuona kama wageni wote wamevikwa mavazi ya arusi, vazi safi (lisilokuwa na mawaa) la tabia iliyosafishwa katika damu ya Mwana-Kondoo. Ufunuo 7:14, Wote ambao kwa uchunguzi wameonekana kuwa wamevaa vazi la arusi wamekubaliwa na kuhesabiwa haki ya kupata sehemu katika ufalme wa Mungu na kukaa kwa kiti chake cha enzi. Kazi hii ya uchunguzi wa tabia ni hukumu ya uchunguzi, kazi ya mwisho ndani ya Pahali patakatifu kule mbinguni.TSHM 206.3

  Wakati mambo ya wale katika vizazi vyote waliokubali Kristo yanapokwisha kuchunguzwa na kukatwa, ndipo rehema itafungwa na mlango wa rehema utafungwa. Kwa hivyo kwa maneno mafupi ya hukumu, “Nao waliokuwa tayari waliingia pamoja naye kwa arusi: mlango ukafungwa,” tumechukuliwa chini kwa wakati ambao kazi kubwa kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu itakapokamilika.TSHM 206.4

  Katika Pahali patakatifu pa kidunia, wakati kuhani mkubwa kwa Siku ya Upatanisho alipoingia kwa Pahali patakatifu pa patakatifu, huduma ndani ya chumba cha kwanza ulimalizika. Vivyo wakati Kristo alipoingia kwa Pahali patakatifu pa patakatifu kufanya kazi ya kumaliza upatanisho, alimaliza huduma yake katika chumba cha kwanza. Ndipo huduma katika chumba cha pili ikaanza. Kristo ametimiza tu sehemu moja ya kazi yake kama mwombezi wetu, ili kuingia kwa sehemu ingine ya kazi. Alikuwa akiendelea kutetea damu yake mbele ya Baba kwa ajili ya wenye zambi.TSHM 206.5

  Kwa hivi inakuwa kweli kwamba mlango ule wa tumaini na rehema ambazo watu walikuwa nazo kwa miaka 1800 walipata ruhusa ya kukaribia kwa Mungu ulifungwa, mlango mwingine ukafunguliwa. Msamaha wa zambi ukatolewa kwa njia ya uombezi wa Kristo ndani ya Pahali patakatifu pa patakatifu mno,. Hapo kukingali na “mlango wazi” kwa Pahali patakatifu pa mbinguni, mahali Kristo alikuwa akifanya kazi kwa ajili ya mwenye zambi.TSHM 207.1

  Sasa ikaonekana matumizi ya yale maneno ya Kristo katika Ufunuo, yanayosemwa kuelekea wakati huu kabisa: “Maneno haya anasema aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi; naye anayefungua wala hapana mtu anayefunga, naye anafunga wala hapana mtu anayefungua .... Tazama, nimekupa mlango wazi mbele yako na hakuna mtu anayeweza kuufunga.” Ufunuo 3:7,8.TSHM 207.2

  Wale ambao kwa imani wanamufuata Yesu katika kazi kubwa ya upatanisho wanapokea faida ya uombezi, huku wale wanaokataa nuru hawatapata faida. Wayuda waliokataa kuamini Kristo kama Mwokozi hawakuweza kupokea rehema kwake. Wakati Yesu alipopanda mbinguni aliingia Pahali patakatifu pa mbinguni kutoa mibaraka ya upatanisho wake juu ya wanafunzi wake, Wayuda waliachwa katika giza kubwa kabisa kwa kuendelea na kafara zao zabure na sadaka. Mlango ambao watu walipata mbele kwa kupita na kumukaribia Mungu haukuwa wazi tena. Wayuda walikataa kumutafuta kwa njia moja tungaliweza kupatikana, ni kwa njia ya Pahali patakatifu pa mbinguni.TSHM 207.3

  Wayuda wasioamini walionyesha uvivu na kutoamini kwa waliojidai kuwa Wakristo ambao kwa kweli hawajui kazi ya Kuhani wetu Mkuu. Katika kazi ya mfano, wakati kuhani mkuu alipoingia Pahali patakatifu pa patakatifu mno, Israeli yote ililazimishwa kukusanyika kwa Pahali patakatifu na kunyenyekeza roho zao mbele ya Mungu, ili waweze kupata rehema ya zambi na bila “kukatiliwa mbali” ya kusanyiko. Ni kwa maana gani tena siku hii ya mfano wa upatanisho ikiwa kwamba tunafahamu kazi ya kuhani wetu Mkuu na kujua kazi gani tunazo ombwa.TSHM 207.4

  Ujumbe ulitumwa kutoka mbinguni kwa dunia katika siku za Noa, na wokovu wao ulitegemea namna gani walitendea ujumbe ule. Mwanzo 6:6-9, Waebrania 11:7. Katika wakati wa Sodomo, wote ila Loti pamoja na mke wake na mabinti wawili, wakateketezwa na moto uliotumwa chini kutoka mbinguni. Mwanzo 19. Vivyo hivyo katika siku za Kristo. Mwana wa Mungu akatangaza kwa Wayuda wasioamini: “Nyumba yenu imeachwa kwenu tupu.” Matayo 23:38. Kutazama chini kwa siku za mwisho, nguvu isiyokuwa na mwisho ya namna moja inatangaza, kwa ajili ya wale ambao “hawakupokea upendo wa kweli, wapate kuokolewa”. “Na kwa ajili ya hiyo Mungu anawaletea nguvu ya upotevu, hata waamini uwongo.” 2 Watesalonika 2:10,11. Kwa sababu wanakataa mafundisho ya neno lake, Mungu anaondoa Roho yake na kuwaacha kwa udanganyifu wanaoupenda. Lakini Kristo akingali anaomba kwa ajili ya mwanadamu, na nuru itatolewa kwa wale wanaoitafuta.TSHM 207.5

  Kupita kwa wakati katika mwaka 1844 ulifuatwa na jaribio kubwa kwa wale walioshika imani ya kuja kwa Yesu. Msaada wao ulikuwa nuru ambayo iliongoza mioyo yao kwa Pahali patakatifu pa mbinguni. Kwa namna walivyongojea na kuomba wakaona kwamba kuhani wao Mkuu alikuwa akiingia kwa kazi ingine ya huduma. Kumufuata kwa imani, wakaongozwa kuona vilevile kufungwa kwa kazi ya kanisa. Wakawa na maelezo kamili zaidi ya ujumbe wa malaika wa kwanza na wa pili, na wakatayarishwa kupokea na kutoa kwa dunia onyo kubwa la malaika wa tatu wa Ufunuo 14.TSHM 208.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents