Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    38 / UJUMBE WA MUNGU ULIO WA MWISHO

    “Nyuma ya maneno haya nikaona malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kubwa; na dunia ikangazwa kwa utukufu wake. Akalia kwa sauti kubwa, akisema: Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkubwa, umekuwa makao ya mashetani, na boma la kila pepo mchafu na boma la kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;TSHM 294.1

    Na nikasikia sauti nyingine toka mbinguni ikisema: Tokeni kwake, watu wangu, musishirikiane na zambi yake, wala musipokee mapigo yake”. Ufunuo 18:1,2,4.TSHM 294.2

    Matangazo yaliyofanywa na malaika wa pili ya Ufunuo 14 (fungu 8) ni ya kukaririwa, pamoja na mtajo mwingine wa machafuko yaliokuwa yakiingia katika Babeli tangu ujumbe ulipotolewa mara ya kwanza.TSHM 294.3

    Hali ya kitisha inaelezwa hapa. Kwa kila kukataa kwa ukweli akili za watu zitakuwa giza sana, mioyo yao mikaidi zaidi. Wataendelea kukanyanga mojawapo ya maagizo ya amri kumi hata wanapotesa wale wanaoishika kuwa takatifu. Kristo anawekwa kwa sifuri juu ya zarau lililowekwa kwa Neno lake na kwa watu wake.TSHM 294.4

    Ungamo la dini litakuwa ni tendo la kudanganya kwa kuficha uovu wa msingi kabisa. Uaminifu katika imani ya kuwa roho za watu waliokufa hurudi na kujionyesha na kuongea na watu (spiritualisme) inafungua mlango kwa mafundisho ya mashetani, na kwa hivyo mvuto wa malaika wabaya utaonekana katika makanisa. Babeli umejaza kipimo cha zambi zake, na maangamizo ni karibu kuanguka.TSHM 294.5

    Lakini Mungu akingali na watu katika Babeli, na waaminifu hawa wanapashwa kuitwa kutoka ili wasishirikiane na zambi zake na “wasipokee mapingo yake”. Malaika anashuka toka mbinguni kuangazia dunia kwa utukufu wake na kutangaza zambi za Babeli. Mwito umesikilika: “Tokeni kwake, watu wangu”. Matangazo haya yanakuwa onyo ya mwisho kutolewa kwa wakaaji wa dunia.TSHM 294.6

    Nguvu za dunia, kuungana kwa vita kupinga amri za Mungu, zitaamuru ya kama “wote, wadogo na wakubwa, na matajiri na masikini na wahuru na wafungwa” (Ufunuo 13:16) watakubali desturi za kanisa kwa kushika sabato ya uwongo. Wote wanaokataa mwishoni watatangazwa wenye kustahili mauti. Kwa upande mwingine, sheria ya Mungu inaagiza siku ya pumziko ya Mungu inaonya hasira juu ya wote wanaovunja amri zake.TSHM 294.7

    Kwa matokeo, ndivyo ilivyoletwa wazi mbele yake, ye yote atakayekanyanga juu ya sheria ya Mungu na kutii sheria ya kibinadamu anapokea alama ya mnyama, ishara ya uaminifu kwa uwezo anaouchagua kutii badala ya Mungu. “Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, yeye naye atakunywa katika mvinyo wa gazabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake”. Ufunuo 14:9,10.TSHM 294.8

    Hakuna mmoja anayeteseka na hasira ya Mungu mpaka kweli inapokwisha kuletwa nyumbani kwa moyo wake na zamiri na inapokataliwa. Wengi hawakupata kamwe bahati ya kusikia mambo ya ukweli wa kipekee kwa wakati huu. Yeye anayesoma kila moyo hataacha mmoja anayetamani kweli kudanganywa kama matokeo ya mashindano. Kila mmoja anapashwa kuwa na nuru ya kutosha kufanya mpango wake kwa akili.TSHM 295.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents