Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mfalme wa Wafalme Anatokea

  Sauti ya Mungu imesikilika kutangaza siku na saa ya kuja kwa Yesu. Israeli wa Mungu anasimama kwa kusikiliza, nyuso zao zikaangaziwa na utukufu wake. Karibu pale kukatokea kwa upande wa mashariki wingu nyeusi dogo. Ni wingu linalomzunguka Mwokozi. Kwa utulivu wa heshima watu wa Mungu wakalitazama kwa namna lilikuwa likikaribia, hata linapokuwa wingu jeupe kubwa, upande wa chini wake ni utukufu kama moto unaoteketeza, na upande wa juu wake upindi wa mvua wa agano. Sasa si “Mtu wa huzuni”, Yesu anapanda (farasi) kama mshindi mkubwa. Malaika watakatifu, makutano makubwa yasiyohesabika, wanamtumikia, “elfu elfu, na elfu kumi mara elfu kumi”. Kila jicho linamwona Mfalme wa uzima. Taji la utukufu linakuwa katika kipaji cha uso wake. Uso wake unashinda (muangaza) wa jua la saa sita. “Naye ana jina llienya kuaandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA”. Ufunuo 19:16.TSHM 311.3

  Mufalme wa wafalme anashuka juu ya wingu, amefunikwa katika moto unaowaka. Dunia inatetemeka mbele yake: “Mungu wetu atakuja, wala hatanyamaza; Moto utakuia mbele yake, Na tufani inayovuma sana itamuzunguka. Ataita mbingu zilizo juu na inchi, ili apate kuhukumu watu wake”. Zaburi 50:3,4.TSHM 312.1

  “Na wafalme wa dunia, na watu mashuhuri, na matajiri, na kila mtumwa, na kila mtu mwenye uhuru wakajificha katika pango na chini ya miamba: Mutuangukie, mutufiche mbele ya uso wake yeye anayeketi juu ya kiti cha ufalme, na gazabu ya Mwana-Kondoo. Kwa maana siku kubwa ya gazabu yake imekuja na nani anayeweza kusimama”? Ufunuo 6:15-17.TSHM 312.2

  Mabishano ya mizaha yamekoma, midomo ya uwongo imenyamazishwa. Hakuna kitu kinachosikiwa lakini sauti ya maombi na sauti ya kilio. Waovu wanaomba kuzikwa chini ya miamba kuliko kukutana na uso wake yeye waliyezarau. Sauti ile iliyoingia kwa sikio la maiti, wanajua. Mara ngapi inakuwa sauti zile za upole ziliwaita kwa toba. Mara ngapi ilikuwa ikisikiwa katika maombi ya rafiki, ya ndugu, ya Mkombozi. Sauti ile inayoamsha ukumbusho wa maonyo yaliyozarauliwa na miito iliyokataliwa.TSHM 312.3

  Kunakuwa wale waliochekelea Kristo katika unyenyekevu wake. Alitangaza: “Tangu sasa mutaona Mwana wa watu akiketi kwa mkono wa kuume wa uwezo, na akija katikati ya mawingu ya mbingu”. Matayo 26:64. Sasa wanamutazama katika utukufu wake; wanapashwa sasa kumwona yeye kukaa kwa mkono wa kuume wa uwezo. Pale kunakuwa Herode mwenye kiburi aliyechekelea cheo chake cha ufalme. Pale panakuwa watu waliomvika taji la miiba juu ya kichwa chake na katika mkono wake fimbo ya kifalme ya kufananisha--wale walioinama mbele yake kwa kutoa heshima ya kumzihaki, waliomtemea mate Mfalme wa uzima. Wanatafuta kukimbia mbele ya uso wake. Wale waliopigilia misumari kwa mikono yake na miguu wanatazama alama hizi kwa hofu na majuto.TSHM 312.4

  Kwa hofu ya wazi wazi makuhani na watawala wanakumbuka matukio ya Kalvari, namna gani, walipotikisa vichwa vyao katika shangwe ya uovu wa Shetani, wakapaaza sauti, “Aliokoa wengine; hawezi kujiokoa yeye mwenyewe”. Matayo 27:42. Kwa sauti kubwa kuliko kelele, “Asulibiwe, asulibiwe”! ambayo ikavuma katika Yerusalema, inaongeza maombolezo ya kukata tamaa, ‘’Yeye ni Mwana wa Mungu”! Wanatafuta kukimbia mbele ya uso wa Mfalme wa wafalme.TSHM 312.5

  Katika maisha ya wote wanaokataa kweli kunakuwa na nyakati ambapo zamiri inaamka, wakati nafsi inaposumbuliwa na masikitiko ya bure. Lakini mambo haya ni nini kulinganisha na majuto ya siku ile! Katikati ya hofu kuu yao wanasikia watakatifu kupaaza sauti: “Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Tuliyemungoja, naye atatuokoa”. Isaya 25:9.TSHM 313.1

  Sauti ya Mwana wa Mungu inaita kwa kuamsha watakatifu wanaolala. Po pote duniani wafu watasikia sauti ile, na wale wanaoisikia wataishi, jeshi kubwa la kila taifa, na kabila na lugha na jamaa. Kutoka kwa nyumba ya gereza ya wafu wanakuja, wanapovikwa utukufu wa milele, kupaaza sauti: “Ee mauti, kushinda kwako ni wapi? Ee mauti, uchungu wako ni wapi”? 1 Wakorinto 15:55.TSHM 313.2

  Wote wanaamka kutoka makaburini wakiwa kwa hali ileile waliyopoingia nayo kaburini. Lakini wote wanafufuka pamoja na upya na nguvu za ujana wa milele. Kristo alikuja kurudisha na kuponya kile kilichopotea. Atabadilisha miili yetu ya unyonge na kuzifanya kama wake mwili mtukufu. Mwili wa mauti na wa kuharibika, mara moja unaoharibika na zambi, unakuwa sasa kamilifu, mzuri na wa kuishi milele. Madoo na ulema vimebaki ndani ya kaburi. Waliokombolewa “watakua” (Malaki 4:2) kwa kimo kamili cha uzao katika utukufu wake wa kizazi cha kwanza, alama za mwisho za laana za zambi zimeondolewa. Waaminifu wa Kristo wataonyesha mfano kamili wa Bwana wao katika roho na nafsi na mwili.TSHM 313.3

  Wenye haki walio hai wamebadilika “kwa dakika moja, kwa kufunga na kufungua kwa jicho”. Kwa sauti ya Mungu wamefanywa watu wa maisha ya milele na pamoja na watakatifu waliofufuka watachukuliwa juu kumlaki Bwana wao katika mawingu. Malaika “watakusanya wachaguliwa wake toka pepo ine, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho mwingine”. Matayo 24:31. Watoto wadogo wamechukuliwa kwa mikono ya mama zao. Rafiki walioachana wakati mrefu kwa ajili ya mauti wameunganika, hakuna kuachana tena kamwe, na pamoja na nyimbo za furaha wanapanda pamoja kwa mji wa Mungu.TSHM 313.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents