Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mwito wa Calvin

  Katika mojawapo ya mashule ya Paris, kulikuwa kijana mmoja mwangalifu, mtulivu, kijana aliyeonekana na maisha yasiyokuwa na kosa, kwa ajili ya bidii ya elimu na kwa ajili ya ibada ya dini. Tabia yake na matumizi vikamufanya kuwa majivuno ya chuo kikubwa, na ilikuwa ikitumainiwa kwa siri kwamba Jean Calvin angekuwa mmojawapo miongoni mwa watetezi wenye uwezo sana, wa kanisa. Lakini mshale wa nuru ukaangazia kuta za elimu nyingi na ibada ya sanamu ambayo Calvin amajifungia. Olivetan, binamu mtoto wa ndungu wa Calvin, alijiunga na Watengenezaji. Ndugu hawa wawili wakazungumza pamoja juu ya maneno ambayo yanasumbua jamii la kikristo. “Hapo kuna dini mbili tu ulimwenguni,” akasema Olivetan, Mprotestanti. “Ile ... ambayo watu wamevumbua, ambamo mtu hujiokoa mwenyewe kwa sherehe na kazi nzuri; ingine ni ile dini ambayo inayofunuliwa katika Biblia, na ambayo hufundisha mtu kutumaini wokovu tu kwa neema bila bei kutoka kwa Mungu.”TSHM 101.2

  “Sitaki mafundisho yenu mapya,” akajibu Calvin; “Unafikiri kwamba nimeishi katika kosa siku zangu zote?” Lakini peke yake chumbani akatafakari maneno ya binamu (cousin) wake. Akajiona mwenyewe kuwa bila mpatanishi mbeie ya Mhukumu mtakatifu na wa haki. Matendo mazuri, sherehe za kanisa, yote yalikuwa bila uwezo kwa upatanisho kwa ajili ya zambi. Ungamo, kitubio, hayakuweza kupatanisha roho pamoja na Mungu.TSHM 101.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents