Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mwisho Mkali Sana wa Waovu

  Tabia ya Shetani inaendelea bila kubadilika. Uasi kama maji mengi yenye kupita kwa nguvu tena yamejipenyeza kwa nguvu. Anakusudia kutoacha vita yenye kukata tamaa ya mwisho ya kupambana na Mfalme wa mbinguni. Lakini kwa mamilioni isiyohesabika yote ambayo aliyoshawishi katika uasi, hakuna anayekubali sasa mamlaka yake. Waovu wamejazwa na uchuki wa namna moja kwa Mungu unaoongozwa na Shetani, lakini wanaona ya kwamba hoja lao halina matumaini. “Kwa sababu umeweka moyo wako kama moyo wa Mungu, kwa hivi, tazama, nitaleta wageni juu yako, watu wa mataifa wenye kuogopesha, na watachomoa panga zao juu ya uzuri wa hekima yako, nao watatia uchafu kungaa kwako. Watakuleta chini kwa shimo. ... nitakuharibu, Ee kerubi la kufunika, kutoka katikati ya mawe ya moto... nitakutupa hata inchi, nitakulaza mbele ya wafalme, wapate kukuona ... nitakufanya kuwa majivu juu ya inchi mbele ya wote wanaokutazama ... utakuwa maogopesho, wala hutakuwa tena hata milele”. Ezekieli 28:6-8, 16-19.TSHM 328.2

  “Maana kasirani kali ya Bwana ni juu ya mataifa yote”. “Atanyeshea waovu mitego; Moto na kiberiti na upepo wa kuchoma zitakuwa fungu la kikombe chao”. Isaya 34:2; Zaburi 11:6. Moto utashuka kutoka kwa Mungu mbinguni. Dunia itaharibika. Miako ya moto unaoteketeza inatoka kwa nguvu kutoka kwa kila shimo kubwa linalokuwa wazi. Miamba halisi inakuwa motoni. Na viumbe vya asili vitayeyushwa kwa moto mkali, na inchi na kazi zilizo ndani yake zitateketea. 2 Petro 3:10. Uso wa dunia utaonekana kama fungu moja kubwa lililoyeyuka--, ziwa la moto lililochafuka. Maana ni “siku ya kisasi cha Bwana, mwaka wa malipo, kwa ubishi wa Sayuni”. Isaya 34:8.TSHM 328.3

  Waovu wanaazibiwa “kama ilivyo kazi yao”. Shetani atateswa si kwa ajili ya uasi wake pekee, bali kwa ajili ya zambi zote alizozilazimisha watu wa Mungu kuzitenda. Katika ndimi za moto waovu watakuwa kwa maangamizi ya mwisho, shina na matawi-Shetani ni shina lenyewe na wafuasi wake ni matawi. Azabu kamili ya sheria ilijiliwa; matakwa ya haki yametimizwa. Kazi ya Shetani ya uharibifu imekomeshwa milele. Sasa viumbe vya Mungu vimekombolewa milele kwa majaribu yake.TSHM 329.1

  Wakati dunia inapofunikwa kwa moto, wenye haki wanakaa kwa salama ndani ya Mji Mutakatifu. Wakati Mungu anakuwa kwa waovu kama moto unaoteketeza, anakuwa ngao kwa watu wake. Tazama Ufunuo 20:6; Zaburi 84:11.TSHM 329.2

  “Nikaona mbingu mpya na dunia mpya; kwa maana mbingu za kwanza na dunia ya kwanza zimekwisha kupita”. Ufunuo 21:1. Moto utakaoteketeza waovu utasafisha dunia. Kila alama ya laana imeondolewa mbali. Hakuna jehanum inayowaka milele itakayoendelea mbele ya waliokombolewa matokeo ya kutisha ya zambi.TSHM 329.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents