Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Matengenezo Katika Danemark

  Katika inchi za kaskazini injili ilipata mwingilio wa amani. Wanafunzi huko Wittenberg waliporudi nyumbani walikuwa wakichukua imani ya matengenezo huko Scandinavia. Maandiko ya Luther pia yakatawanya nuru. Watu hodari wa upande wa kaskazini, wakageuka kutoka maovu na ibada ya sanamu ya Roma na kupokea kwa furaha kweli ya maisha bora ya Biblia.TSHM 111.5

  Tausen, “Mtengenezaji wa Danemark,” kama mtoto mwanzoni, akaonyesha akili ya nguvu na akaingia kwa nyumba ya watawa. Mtihani ulimtambulisha kuwa na talanta iliyoahidi kufanya kazi nzuri kanisani. Mwanafunzi kijana akaruhusiwa kujichagulia mwenyewe chuo kikubwa cha Ujeremani ama cha Uholandi, ila kwa sharti moja tu: hakupashwa kwenda Wittenberg kuhatarishwa na uzushi. Watawa wakasema hivyo.TSHM 111.6

  Tausen akaenda Cologne, mojawapo ya ngome ya Kiroma. Hapo hakukawia kuchukizwa. Ni wakati ule ule aliposoma maandiko ya Luther kwa furaha na akatamani sana kujifunza mafundisho ya kipekee ya Mtengenezaji. Lakini kwa kufanya vile alipashwa kujihatarisha kupoteza usaada wa wakuu wake. Kwa upesi kusudi lake likafanyika na mara akawa mwanafunzi huko Wittenberg.TSHM 112.1

  Kwa kurudi Danemark, hakuonyesha siri yake, lakini akajitahidi kuongoza wenzake kwa imani safi. Akafungua Biblia na akahubiri Kristo kwao kama tumaini pekee la mwenye zambi la wokovu. Hasira ya mkuu wa nyumba ya watawa ilikuwa kubwa sana, walioweka matumaini ya juu juu kwake kuwa mtetezi wa Roma. Akahamishwa mara moja kutoka kwa nyumba yake mwenyewe ya watawa kwenda kwa ingine na kufungiwa kwa chumba chake kidogo. Katika fito za chuma za chumba chake kidogo Tausen akazungumza na wenzake maarifa ya kweli. Kama mababa wema wale wa Danois wangalipatana katika shauri la kanisa juu ya uzushi, sauti ya Tausen haingalisikiwa tena kamwe; lakini badala ya kumzika hai kwa gereza la chini ya udongo, wakafukuzwa kwa nyumba ya watawa.TSHM 112.2

  Amri ya mfalme, ikatangazwa, ikatolea ulinzi kwa elimu ya mafundisho mapya. Makanisa yakafunguliwa kwa ajili yake, na watu wakajaa tele kusikiliza. Agano Jipya katika Kidanois kikaenezwa mahali pengi. Juhudi ya kuangusha kazi ikaishia kwa kuitawanya, na kwa hiyo Danemark ikatangaza ukubali wake wa imani ya matengenezo.TSHM 112.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents