Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Utimilizo wa Ajabu wa Unabii

  Unabii huu ulipata utimilizo wa ajabu katika historia ya Ufransa wakati wa Mapinduzi (Revolution), katika mwaka 1793. “Ufransa ulikuwa ni taifa pekee katika historia ya dunia, ambayo kwa amri ya baraza la sheria, likatangaza kwamba hakuna Mungu, na ambaye wenyeji wote wa mji mkuu, na sehemu kubwa ya watu popote, wanawake na wanaume pia, wakacheza na kuimba kwa furaha kwa kukubali tangazo hili.”TSHM 126.2

  Ufransa ukaonyesha pia tabia ambazo zilipambanua Sodomo. Mwandishi wa historia anaonyesha pamoja kukana Mungu na uasherati wa Ufransa: “Kwa uhusiano na sheria hizi juu ya dini, ilikuwa ile ambayo ilivunja muungano wa ndoa--maagano takatifu kuliko ambayo watu wanaweza kufanya, na kudumu ni wa lazima kwa ulinzi wa jamaa--ukageuzwa kuwa kwa hali ya mapatano ya adabu ya hivi hivi tu ya mda, na kwamba watu wawili wanaweza kuunga na kuvunja kwa mapenzi. ... Sophie Arnoult, mtendaji wa kike wa sifa kwa mambo ya kuchekesha akasema, akaeleza kuwa ndoa ya serkali ni kama `sakramenti ao siri ya uzinzi.’”TSHM 126.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents