Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Berquin kwa Mti Wakufungia Watu wa Kochomwa Moto

    Katika mti Berquin akajitahidi kusema maneno machache kwa watu; lakini watawa wakaanza kupaza sauti na askari kugonganisha silaha zao, na makelele yao yakazamisha sauti ya mfia dini. Hivi kwa mwaka 1529 mamlaka kubwa sana ya kanisa na elimu ya Paris “ikatoa kwa watu wa 1793 mfano wa msingi wa kusongwa juu ya jukwaa (mahali pa kunyongwa) maneno takatifu ya wenye kufa.” Berquin akanyongwa na mwili wake ukateketezwa katika miako ya moto.TSHM 100.5

    Waalimu wa imani ya matengenezo wakaenda katika mashamba mengine ya kazi. Lefévre akaenda Ujermani. Farel akarudi kwa mji wake wa kuzaliwa upande wenashariki ya Ufransa, kutawanya nuru katika makao ya utoto wake. Ukweli aliuofundisha ukapata wasikizaji. Kwa upesi akafukuzwa mbali ya mji. Akapitia vijijini, akifundisha katika makao ya upekee na mashamba ya majani ya uficho, kutafuta kimbilio katika pori na katika mapango ya miamba yaliyokuwa makao yake katika utoto wake.TSHM 100.6

    Kama katika siku za mitume, mateso “yametokea zaidi kwa kuendesha Habari Njema.” Wafilipi 1:12. Walipofukuzwa kutoka Paris na Meaux, “Wale waliosambazwa wakaenda pahali po pote wakihubiri neno.” Matendo 8:4. Ni kwa namna hiyo nuru ilitawanyika mahali pengi katika majimbo ya mbali ya Ufransa.TSHM 101.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents