Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Tetemeko la inchi lililotikisa Ulimwengu

  Kwa kutimilika kwa unabii huu kulitokea katika mwaka 1755 tetemeko la inchi lililokuwa la kutisha zaidi lililoandikwa. Lilijulikana kama tetemeko la inchi la Lisbon, likaenea Ulaya, Afrika, na Amerika. Likasikiwa Groenland, Upande wa Magharibi ya Uhindi, katika Antilles, Norvege na Swede, Uingereza na Irland, kwa eneo si chini kuliko kilometres milioni ine kwa mraba. Katika Afrika mshindo ulikuwa karibu sana wa nguvu kama katika Ulaya. Sehemu Kubwa ya Algiers (Mji mkuu wa Algeria) ikaharibiwa. Wimbi kubwa la kutisha likazamisha pwani ya Espagne na ya Afrika na kudidimiisha miji.TSHM 143.1

  Milima, “ingine katika milima inayo kuwa kubwa sana katika Portugal, ikatikiswa kwa nguvu sana, tangu kwa misingi yao; na ingine kati yao ikafunguka kwa vilele vyao, ambayo ilipasuka na kutengana kwa namna ya ajabu, mafungu makubwa yao kutupwa katika mabonde ya karibu. Ndimi za moto imehadiziwa kutoka kwa milima hizo.”TSHM 143.2

  Huko Lisbon “Sauti ya ngurumo ilisikiwa chini ya udongo, na bila kukawia baadae kishindo kikali kikaangusha sehemu kubwa ya mji ule. Katika mwendo wa dakika karibu sita watu elfu makumi sita wakaangamizwa. Bahari mara ikarudi, na ikaacha kivuko kikavu; na kurudi ndani yake, nakuinuka juu mita makumi tano ao zaidi juu ya daraja lake la kawaida.”TSHM 143.3

  Tetemeko la inchi lilifanyika kwa sikukuu, wakati makanisa na nyumba za watawa zilijaa na watu, wachache sana tu waliokoka.” “Hofu ya watu ilikuwa ya kupita kiasi kwa kuieleza. Hakuna mtu aliyelia; hapakuwa na machozi mbele ya msiba kama huo. Wakakimbia huko na huko, wakipayuka payuka na hofu na mshangao, wakipiga nyuso zao na vifua, kulia, ` Mesericordia! Ni mwisho wa dunia?’ Wamama wakasahau watoto wao, na kukimbia njiani pamoja na sanamu za misalaba. Kwa bahati mbaya, wengi wakakimbilia kwa makanisa kutafuta kimbilio; lakini sacramenti iliwekwa kwa bure; kwa bure viumbe maskini walikumbatia mazabahu; masanamu, mapadri, na watu wakazikwa katika uharibifu moja mbaya wa wote pamoja.”TSHM 143.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents