Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  4 / WAFUASI WA WALDENSE WANAKINGA IMANI

  Katika mda mrefu wa mamlaka ya Papa, kulikuwa washahidi wa Mungu waliolinda imani katika Kristo kama mpatanishi wa pekee kati ya Mungu na mtu. Walishika Biblia kama kiongozi pekee kwa maisha, na kuheshimu Sabato ya kweli. Wakahesabiwa kama wapinga dini, maandiko yao yakakomeshwa, kuelezwa vibaya, ao kuondolewa. Lakini wakasimama imara.TSHM 21.1

  Wanakuwa na nafasi ndogo katika maandiko ya wanadamu, ila tu katika mashitaki ya watesi wao. Kila kitu “cha kupinga dini”, ikiwa ni watu ao maandiko, Roma alitafuta kuharibu. Roma ilijitahidi vile vile kuharibu kila kumbukumbu la maovu wake mbele ya wasiokubali mafundisho yake. Kabla ya uvumbuzi wa ufundi wa kupiga chapa, vitabu vilikuwa vichache kwa hesabu; kwa hiyo juu ya uchache wa vitabu hii haikuzuia Waroma kutimiza kusudi lao. Kanisa la Roma lilipopata uwezo likanyoosha mikono yake kwa kuangamiza wote wale waliokataa kukubali utawala wake.TSHM 21.2

  Katika Uingereza dini ya Kikristo zamani za kale ilikuwa imekwisha kupata mizizi, haikuharibiwa na ukufuru wa Waroma. Mateso ya wafalme wa kipagani yalikuwa tu zawadi ambayo makanisa ya kwanza ya Uingereza yalipata kwa Roma. Wakristo wengi waliokimbia mateso katika Uingereza wakipata kimbilio katika Scotland. Kwa hiyo ukweli ukachukuliwa katika nchi ya Irlande, na katika inchi hizi ukweli ulikubaliwa kwa furaha.TSHM 21.3

  Wakati Wasaxons waliposhambulia Uingereza, upagani ukapata mamlaka, na Wakristo walilazimishwa kukimbilia milimani. Katika Scotland, karne moja baadaye, nuru ikaangazia inchi za mbali sana. Kutoka Irlande Columba akakuja na waidizi wake, waliofanya kisiwa cha pekee cha Iona kuwa makao ya kazi zao za kueneza injili. Miongoni mwa wainjilisti hawa kulikuwa mchunguzi wa Sabato ya Biblia, na kwa hivyo ukweli huu ukaingizwa miongoni mwa watu. Masomo yakaanzishwa pale Iona, ambamo wajumbe (missionnaires) walitoka na kwenda Scotland, Uingereza, Ujeremani, Uswisi, na hata Italia.TSHM 21.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents