Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Wanaongoja Bwana Wao

  Tangazo “Tazama, bwana arusi anakuja” liliongoza maelfu ya watu kutazamia kuja kwa Bwana mara moja. Kwa wakati ulioagizwa Bwana-arusi akaja, si duniani, bali kwa Mzee wa Siku katika mbingu, kwa arusi, kupokelewa kwa ufalme wake. “Nao waliokuwa tayari waliingia pamoja naye kwa arusi.” Hawakupashwa kuwa pale binafsi, kwa sababu wanakuwa duniani. Wafuasi wa Kristo wanapashwa kungojea Bwana wao atakaporudi kutoka arusini. Luka 12:36. Lakini wanapashwa kufahamu kazi yake na kumfuata kwa imani. Kwa nia hii walisemwa kwenda kwa arusi.TSHM 206.1

  Katika mfano, wale waliokuwa na mafuta katika taa zao wakaingia kwa arusi. Wale ambao, katika usiku wa jaribu la uchungu, waliongoja kwa uvumilivu, wakichunguza Biblia kwa ajili ya nuru wazi zaidi--hawa waliona ukweli juu ya Pahali patakatifu katika mbingu na badiliko la huduma ya Mwokozi. Kwa imani wakamfuata katika kazi yake ndani ya Pahali patakatifu juu. Na wote waliokubali kweli zile zile, kumfuata Kristo kwa imani anavyotenda kazi ya mwisho ya upatanisho, wanaingia kwa arusi.TSHM 206.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents