Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ushindani Bora wa Waana wa Wafalme

  Mfalme Ferdinand, mjumbe wa mfalme, akajaribu ufundi wa mvuto. “Akaomba waana wa wafalme kukubali amri, kuwahakikishia kwamba mfalme angependezwa sana nao.” Lakini watu hawa waaminifu wakajibu kwa upole: “Tutamtii mfalme kwa kila kitu kitakacholeta amani na heshima ya Mungu.”TSHM 93.1

  Mwishowe mfalme akatangaza kwamba “njia yao moja tu inayobaki ilikuwa ni kujiweka nchini ya walio wengi.” Alipokwisha kusema basi, akaenda zake, bila kuwapa Watengenezaji nafasi ya kujibu. “Wakatuma ujumbe kusihi mfalme arudi : Akajibu tu, “Ni jambo lilokwisha kukatwa; kutii ni kitu tu kinachobaki.”TSHM 93.2

  Watu wa kundi la mfalme wakajisifu wenyewe kwamba sababu ya mfalme na Papa ilikuwa na nguvu, na kwamba ile ya Watengenezaji ni zaifu. Kama Watengenezaji wangetumainia usaada wa mtu tu, wangalikuwa wazaifu kama walivyo zaniwa na wafuasi wa Papa. Lakini wakaita “kutoka kwa taarifa la baraza kuelekea Neno la Mungu, na badala ya mfalme Charles, kwa Yesu Kristo, Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana.”TSHM 93.3

  Kama vile Ferdinand alivyokataa kujali nia za zamiri yao, watawala wakakusudia bila kujali kukosekana kwake, bali kuleta ushuhuda wao mbele ya baraza la taifa bila kukawia. Tangazo la heshima likaandikwa na kuwekwa kwa mkutano:TSHM 93.4

  “Tunashuhudia kwa wanaokuwa hapa ... kwamba sisi, kwa ajili yetu na kwa ajili ya watu wetu, hatukubali wala kupatana katika namna yote kwa amri iliyokusudiwa, katika kila kitu kinachokuwa kinyume kwa Mungu, kwa Neno lake takatifu, kwa zamiri yetu ya haki, kwa wokovu wa roho zetu ... kwa sababu hii tunakataa utumwa ambao unaotwikwa juu yetu. ... Na vilevile tunakuwa katika matumaini kwamba utukufu wake wa kifalme utatenda mbele yetu kama mfalme Mkristo anayempenda Mungu kupita vitu vyote; na tunatangaza sisi wenyewe kuwa tayari kulipa kwake, na kwenu pia, watawala wa neema, upendo wote na utii unavyokuwa wajibu wetu wa haki na wa sheria.”TSHM 93.5

  Wengi wakajaa na mshangao na mshituko wa hofu kwa ushujaa wa washuhuda. Fitina, ushindano, na kumwaga damu ilionekana bila kuepukwa. Lakini Watengenezaji, katika kutumainia silaha ya mamlaka Kuu, walikuwa wenyekujazwa na “uhodari tele na ujasiri.”TSHM 93.6

  “Kanuni zilizokuwa katika ushuhuda huu wa sifa ... ilianzisha msingi kabisa wa Kiprotestanti. ... Kiprotestanti kinatia uwezo wa zamiri juu ya muhukumu na mamulaka ya Neno la Mungu juu ya kanisa linaloonekana ... Husema pamoja na manabii na mitume “Imetupasa kutii Mungu kuliko mwanadamu. Kuwako kwa taji la Charles V kiliinua taji la Yesu Kristo.” Ushuhuda wa Spires ulikuwa ushuhuda wa heshima juu ya ushupavu wa dini na madai ya haki ya watu wote kwa kuabudu Mungu kwa kupatana na zamiri zao wenyewe.TSHM 94.1

  Maarifa ya Watengenezaji bora hawa yanakuwa na fundisho kwa ajili ya vizazi vyote vinavyofuatana. Shetani angali anapinga Maandiko yaliyofanywa kuwa kiongozi cha maisha. Kwa wakati wetu kuna haja ya kurudi kwa kanuni kubwa ya ushuhuda--Biblia, na ni Biblia peke, kama kiongozi cha amri ya imani na kazi. Shetani angali anatumika kwa kuharibu uhuru wa dini. Uwezo wa mpinga Kristo ambao washuhuda wa Spires walikataa sasa unatafuta kuanzisha mamlaka yake iliyopotea.TSHM 94.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents