Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Badiliko katika Kanisa la Protestanti

  Madai yamewekwa katika inchi za Kiprotestanti ya kwamba Dini ya Kikatoliki inakuwa tofauti kidogo kwa Dini ya Kiprotestanti kuliko nyakati za zamani. Hapo kumekuwa badiliko; lakini badiliko haliko katika kanisa la Roma. Kanisa la Katoliki linafanana sana na Kanisa la Kiprotestanti linalokuwa sasa kwa sababu Kanisa la Kiprotestanti kiliharibika tabia sana tangu siku za Watengenezaji (Reformateurs).TSHM 279.1

  Makanisa ya Kiprotestanti, kutafuta mapendeleo ya ulimwen-gu, yanaamini kila kitu kibaya kuwa kizuri, na kama matokeo wataamini mwishoni kila kitu kizuri kuwa kibaya. Wanakuwa sasa, kama ilivyokuwa, kujitetea kwa Roma kwa ajili ya mawazo yao isiyokuwa na mapendo kwake, kuomba musamaha kwa “ushupavu” wao. Wengi wanasihi sana ya kwamba giza ya kiakili na yakiroho iliyokuwa pote wakati wa Miaka ya Katikati ilisaidia Roma kueneza mambo ya uchawi na mateso, na ya kwamba akili kubwa zaidi ya nyakati za sasa na kuongezeka kwa wema katika mambo ya dini kunakataza mwamsho wa kutovumilia. Watu wanacheka sana wazo la kwamba mambo ya namna ile yanaweza kutokea kwa nyakati za nuru. Inapaswa kukumbukwa lakini ya kwamba kwa namna nuru inapotolewa zaidi, na zaidi giza ya wale wanaopotea na kuikataa itakuwa kubwa.TSHM 279.2

  Siku ya giza kubwa ya walio elimishwa imesaidia kwa mafanikio ya kanisa la Roma (Papa). Siku ya nuru kubwa ya walioelimishwa nayo itasaidia vile vile. Katika miaka iliyopita wakati watu walipokuwa pasipo maarifa ya ukweli, maelfu walikamatwa kwa mtego, bila kuona wavu uliotandikwa kwa nyanyo zao. Katika kizazi hiki wengi hawatambui wavu na wanatembea ndani yake mara moja bila kufikiri. Wakati watu wanapotukuza mafundisho yao wenyewe juu ya Neno la Mungu, akili inaweza kutimiza maumivu makubwa kuliko ujinga. Kwa hivyo elimu ya uwongo ya wakati huu utahakikisha mafanikio ya kutayarisha njia kwa kukubali kanisa la Roma (Papa), kama kukataa kwa maarifa kulivyofanya katika Miaka ya Giza.TSHM 279.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents