Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mwenendo wa Salama Kutoka kwa Mfalme

    Katika barua kwa rafiki zake akasema: “Ndugu zangu, ... nimefanya safari pamoja na mwenendo wa usalama kutokuwa ya mfalme kwakukutana na maadui wangu wengi wa kibinadamu. ... Yesu Kristo aliteswa kwa ajili ya wapenzi wake; na kwa hiyo hatupaswe kushangazwa kwamba alituachia mfano wake? ... Kwa hiyo, wapenzi, kama kifo changu kinapaswa kutoa sehemu kwa utukufu wake, naomba kwamba kipate kunifikia upesi, na kwamba aweze kuniwezesha kuvumilia mateso kubwa yangu yote kwa uaminifu. ... Hebu tuombe kwa Mungu ... kwamba nisipate kuvunja haki hata ndogo ya ukweli ya injili, ili nipate kuacha mfano bora utakao fuatwa na ndugu zangu.”TSHM 42.3

    Katika barua ingine, Huss alisema kwa unyenyekevu wa makosa yake mwenyewe, kujishitaki mwenyewe “kwa kupendezwa kwa kuvaa mavazi ya utajiri na kuweza kupoteza wakati katika shuguli zisizo na maana.” Ndipo akaongeza, “hebu utukufu wa Mungu na wokovu wa mioyo utawale akili yako, na si upato wa faida na mashamba. Epuka kuipamba nyumba yako zaidi ya roho yako; na, juu ya yote, toa uangalifu wako kwa kiroho. Uwe mtawa na mpole na maskini, na usimalize chakula chako katika kufanya karamu.”TSHM 43.1

    Huko Constance, Huss alipewa uhuru kamili. Kwa mwenendo wa salama wa mfalme kuliongezwa uhakikisho wa ulinzi wa Papa. Lakini, katika mvunjo wa metangazo haya yaliyokuwa yakikaririwa, kwa mda mfupi Mtengenezaji akufungwa kufuatana na agizo la Papa na wakuu (cardinals) na kusukumwa ndani ya gereza mbaya la chini ya ngome. Baadaye akahamishwa kwa ngome ya nguvu ngambo ya mto Rhine na huko mfungwa alikuwa akilindwa. Papa kwa upesi baadaye akawekwa kwa gereza ile ile. Alishuhudiwa kuwa mwenye hatia ya makosa mabaya, kuua mtu kwa kusudi zaidi, kufanya biashara ya mambo matakatifu ya dini, na uzinzi, “zambi zisizofaa kutajwa.” Baadaye akanyanganywa taji lake. Mapapa wapinzani pia wakaondolewa, na askofu mpya akachaguliwa.TSHM 43.2

    Ingawa pape mwenyewe alikuwa mwenye hatia ya makosa makubwa kuliko Huss aliyoyaweka juu ya mapadri, bali ni baraza lile lile lililoondoa cheo cha askofu likadai kuangamiza Mtengenezaji. Kifungo cha Huss kikaamsha hasira nyingi katika Bohemia. Mfalme, alipokataa kuvunja mwenendo wa usalama, akapinga mambo juu yake. Lakini maadui wa Mtengenezaji wakaendelea kuleta mabishano kushuhudia kwamba “imani haipaswi kushikwa pamoja na asiyefundisha makwa ya kanisa ao mtu anayezaniwa na upinzani wamafundisho ya kanisa, hata wakiwa watu wanoakuwa na mwenendo wa usalama kutoka kwa mfalme na wafalme.”TSHM 43.3

    Kuwa mzaifu sababu ya ugonjwa-gereza lenye baridi na maji maji likaleta homa ambayo karibu kumaliza maisha yake-mwishowe Huss akaletwa mbele ya baraza. Mwenye kufungwa minyororo akasimama mbele ya mfalme, ambaye juu ya imani nzuri aliyokuwa nayo aliaahidi kumlinda. Akashikilia ukweli kwa nguvu na kutoa ushuhuda wa kutokubali maovu ya waongozi wa dini. Akashurutishwa kuchagua au kukana mafundisho yake ao kuuwawa, akakubali kifo cha wafia dini.TSHM 43.4

    Neema ya Mungu ikamsaidia. Mda wa juma ya kuteseka kabla ya hukumu ya mwisho, amani ya mbinguni ikajaa rohoni mwake. “Ninaandika barua hii”, akasema kwa rafiki, “katika gereza langu, na mkono wangu katika minyororo, kutazamia hukumu yangu ya kifo kesho. ... Wakati, kwa msaada wa Yesu Kristo, tutakutana tena katika amani ya kupendeza sana ya maisha yajayo, mtajifunza namna gani Mungu wa rehema amejionyesha mwenyewe mbele yangu, namna gani ya kufaa amenisaidia katikati ya majaribu na mashindano yangu.”TSHM 44.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents