Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ushahidi kwa Mchomo

  Calvin akapitia siku moja katika uwanja mkubwa, kwa bahati njema akaona mpinga ibada ya dini anapokufa kwa moto. Miongoni mwa mateso ya kifo cha kuhofisha na chini ya kukatiwa hukumu kwa kanisa, mfia dini akaonyesha imani na uhodari ambao mwanafunzi kijana kwa uchungu aliona ni kinyume kwa ukosefu wa tumaini lake mwenyewe na giza. Juu ya Biblia, alijua, “wazushi” walidumisha imani yao. Akakusudia kujifunza Biblia yenyewe na kuvumbua siri ya furaha yao.TSHM 101.4

  Ndani ya Biblia akampata Kristo. “Ee Baba,” akalia, “Kafara yake ilituliza hasira yako; Damu yake imesafisha takataka zangu; Msalaba wake ulichukua laana yangu; Mauti yake ilitoa kafara kwa ajili yangu. ... Umegusa moyo wangu, ili niweze kusimama katika matendo mema mengine yote kama mahukizo isipokuwa matendo mema ya Yesu.TSHM 102.1

  Sasa akakusudia kutoa maisha yake kwa injili. Lakini kwa tabia alikuwa mwenye woga na alitamani kujitoa mwenyewe kujifunza. Maombi ya bidii ya rafiki zake, lakini, mwishowe yakashinda ukubali wake kwa kuwa mwalimu wa watu wote. Maneno yake yalikuwa kama umande unaoanguka kwa kuburudisha udongo. Alikuwa sasa katika mji wa jimbo chini ya ulinzi wa binti kifalme Margeurite, ambaye, kwa kupenda injili, akaeneza ulinzi wake kwa wanafunzi wake. Kazi ya Calvin ikaanza pamoja na watu nyumbani mwao. Wale waliosikia ujumbe wakachukua Habari Njema kwa wengine. Akaendelea, kuweka msingi wa makanisa yaliyopaswa kutoa ushuhuda hodari kwa ajili ya ukweli.TSHM 102.2

  Mji wa Paris ulipashwa kupokea mwaliko mwengine kwa kukubali injili. Mwito wa Lefévre na Farel ulikataliwa, lakini ujumbe ulipashwa kusikiwa tena kwa vyeo vyote katika mji mkuu ule. Mfalme alikuwa hajakamata mpango wa kuwa upande wa Roma kupinga Matengenezo. Margeurite (dada yake) alitamani kwamba imani ya Matengenezo ihubiriwe katika Paris. Akaagiza mhubiri wa Kiprotestanti kuhubiri katika makanisa. Jambo hili likakatazwa na mapadri wa Papa, binti mfalme akafungua jumba. Ikatangazwa kwamba kila siku hotuba inapaswa kufanyika, na watu wakaalikwa kuhuzuria. Maelfu wakakusanyika kila siku.TSHM 102.3

  Mfalme akaagiza kwamba makanisa mawili ya Paris yalipaswa kufunguliwa. Kamwe mji ulikuwa haujavutwa na Neno la Mungu kama wakati ule. Kiasi, usafi, utaratibu, na utendaji, mambo yale yakachukua pahali pa ulevi, uasherati, shindano, na uvivu. Weakati walikubali injili, walio wengi wa watu wakaikataa. Wakatoliki wakafaulu kupata tena uwezo wao. Tena makanisa yakafungwa na mti wa kufungia watu wakuchomwa ukasimamishwa.TSHM 102.4

  Calvin alikuwa akingali Paris. Mwishowe mamlaka ikakusudia kumleta kwa ndimi za moto. Hakuwa na mawazo juu ya hatari wakati rafiki walikuja kwa haraka kwa chumba chake na habari kwamba wakuu walikuwa njiani mwao kumfunga. Kwa wakati ule sauti ya bisho likasikiwa kwa mlango wa inje. Hapo hapakuwa na wakati wa kupoteza. Rafiki wakakawisha wakuu mlangoni na wengine wakasaidia Mtengenezaji kumshusha chini kwa dirisha, na kwa haraka akaenda kwa nyumba ndogo ya mtu wa kazi aliyekuwa rafiki wa Matengenezo. Akajigeuza mwenyewe kwa mavazi ya mwenyeji wake na, kuchukua jembe mabegani, akaanza safari yake. Akasafiri upande wa Kusini, akapata tena kimbilio katika utawala wa Margeurite.TSHM 102.5

  Calvin hakuweza kubakia wakati mrefu bila kazi. Mara msukosuko ulipotulia akaenda kutafuta shamba mpya ya kazi huko Poities, mahali makusudi mapya yalikuwa ya kufaa kukubaliwa. Watu wa namna zote walisikiliza kwa furaha habari njema. Kwa namna hesabu ya wasikilizaji ilivyokuwa ikiongezeka, wakafikiri kwamba ni vyema kukusanyikia inje ya mji. Kwa pango mahali miti na miamba ya juu ya uficho pakachaguliwa kuwa mahali pa mkutano. Katika mahali hapa pa uficho Biblia ikasomwa na kufasiriwa. Hapo ibada ya meza ya Bwana ikafanyika kwa mara ya kwanza kwa Waprotestanti wa Ufransa. Kwa kanisa ndogo hilo kukatoka wahubiri wengi waaminifu.TSHM 103.1

  Mara ingine tena Calvin akarudi Paris, lakini akakuta karibu kila mlango wa kazi umefungwa. Yeye mwishowe akakusudia kwenda Ujeremani. Kwa shida aliacha Ufransa wakati zoruba ilitokea juu ya Waprotestanti. Watengenezaji wa Ufransa wakakusudia kupambana na pigo hodari juu ya mambo ya ibada ya sanamu ya Roma ile iliyopashwa kuamsha taifa lote. Matangazo kwa kushambulia misa katika usiku moja yakawekwa kwa Ufransa pote. Mahali pa kuendeleza kazi ya Matengenezo, tendo hilo la upumbavu likawapa Warumi sababu ya kudai kuangamizwa kwa “wapinga ibada ya dini” kama wafitini wa hatari kwa usitawi wa kiti cha mfalme na amani ya taifa.TSHM 103.2

  Mojawapo ya matangazo liliwekwa kwa mlango wa chumba cha pekee cha mfalme. Uhodari wa upekee wa kujiingiza kwa maneno ya kushangaza haya mbele ya mfalme na jambo hilo likaamsha hasira ya mfalme. Ghazabu yake ikapata usemi katika maneno makali: “Wote wakamatiwe bila tofauti wanaozaniwa kuwa wafuasi wa Luther. Nitawaangamiza wote.” Mfalme akajiweka kwa upande wa Roma.TSHM 103.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents