Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mabishano kwa Ajiii ya Mtu

  Mbingu yote ikaona haki ya Mungu kufunuliwa. Lusifero alidai kwamba wanadamu wa zambi wangekuwa mbali ya ukombozi. Lakini azabu ya sheria ikaanguka juu yake aliyekuwa sawa na Mungu, na mtu akawa huru kukubali haki ya Kristo na kwa njia ya toba na kujishusha kwa kushinda nguvu za Shetani.TSHM 244.2

  Lakini Kristo hakuja duniani kufa kwa ajili ya kukomboa mtu tu. Alikuja kuonyesha kwa dunia zote kwamba sheria ya Mungu ni sheria isiyobadilika. Mauti ya Kristo inaihakikisha kuwa isiyogeuka na inaonyesha kwamba haki na rehema ndiyo msingi wa utawala wa Mungu. Katika hukumu ya mwisho itaonekana kwamba hapana sababu kwa ajili ya zambi kuwako. Wakati Mwamzi wa dunia yote atakapo muuliza Shetani, “Sababu gani uliasi juu yangu?” Mwanzishaji wa zambi hataweza kutoa sababu.TSHM 244.3

  Katika kupaza sauti kwa Mwokozi, “Imekwisha, “tarumbeta ya mauti ya Shetani ililia. Vita kuu ikakusudiwa, kungoa kwa mwisho kwa uovu kukahakikishwa. Kwa maana “siku inakuja, inawaka kama tanuru; na wenye kiburi wote, na wote wanaotumika uovu watakuwa kama makapi makavu; na siku itakayokuja itawateketeza, Bwana wa majeshi anasema; hata haitawaachia, wala shina wala tawi.” Malaki 4:1. Uovu hautaonekana tena kamwe. Sheria ya Mungu itaheshimiwa kama sheria ya uhuru. Viumbe vyote vilivyojaribiwa na kuhakikishwa havitageuka kamwe kwa kumtii yeye ambaye tabia yake imeonekana kama upendo usiopimika na hekima isiyo na mwisho.TSHM 244.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents