Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Malaika wa Mauti

  Sasa malaika wa mauti anaenda mbele, anaonyeshwa katika ndoto ya Ezekieli kwa watu wanaokuwa na silaha za kuchinja, kwao agizo limetolewa: “Ueni kabisa mzee na kijana, na wote wawili wasichana, na watoto wadogo, na wanawake, lakini musikaribie mtu aliye na alama ile juu yake; na anzieni kwa pahali pangu patakatifu”, ‘’halafu wakaanza kwa wazee walio mbele ya nyumba, “wale waliojidai kuwa walinzi wa kiroho wa watu. Ezekieli 9:6.TSHM 319.2

  Walinzi wa uwongo wanakuwa wa kwanza kuanguka. “Kwa maana tazama, Bwana anakuja kutoka pahali pake kuazibu wenye kukaa duniani kwa sababu ya uovu wao; na dunia itafunua damu yake, na haitafunika tena watu wake waliouawa”. “Na itakuwa siku ile makelele makubwa toka kwa Bwana yatakuwa katikati yao; nao watakamata kila mtu mkono wa jirani yake, na mkono wake utanyanyuliwa juu ya mkono wa jirani yake” Isaya 26:21; Zekarai 14:13.TSHM 319.3

  Katika vita yenye wazimu ya tamaa kali zao wenyewe na kwa kumiminika kwa gazabu ya Mungu isiyo changanywa, wakuhani waovu wanaanguka, watawala, na watu. “Na waliouawa wa Bwana siku ile watakuwa toka mwisho wa dunia hata mwisho wa dunia”. Yeremia 25:33.TSHM 319.4

  Kwa kuja kwa Kristo waovu wataangamizwa kwa mwangaza wa utukufu wake. Kristo atachukua watu wake kwa mji wa Mungu, na dunia itafanyiwa utupu kwa wakaaji wake. “Tazama Bwana anafanya dunia kuwa utupu, na anaiharibu, na anaipindua, na kuwasambaza popote wakaaji wake... Inchi itafanywa kuwa utupu kabisa, na kuharibiwa kabisa; kwa maana Bwana amesema neno hili... kwa sababu wamevunja sheria, wamegeuza amri, wamevunja agano la milele. Kwa sababu hii laana imekula dunia, na watu wanaokaa ndani yake wanaonekana kuwa na laumu: kwa hivi wakaaji wa dunia wamechomwa”. Isaya 24:1,3,5,6.TSHM 319.5

  Dunia inaonekana kama jangwa lenye ukiwa. Miji imeharibiwa na tetemeko, miti kungolewa, miamba iliyopasuka duniani imetawanyika juu ya uso wa dunia. Mapango makubwa yanaonyesha alama mahali milima ilipasuka kutoka kwa misingi yao.TSHM 320.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents