Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mpinga Mbiu wa Wakati wa Sasa

  Mungu alitia neno la ukweli katika kinywa cha Wycliffe. Maisha yake yalilindwa na kazi zake zikazidishwa hata msingi ukawekwa kwa ajili ya Matengenezo (Reformation). Hapakuwa mtu aliyekwenda mbele ya Wycliffe ambaye kwa kazi yake aliweza kutengeneza utaratibu wake wa matengenezo. Alikuwa mpinga mbiuwa wakati wa sasa. Bali katika ukweli ambayo alioonyesha, kulikuwa umoja na ukamilifu ambao watengenezaji waliofuata hawakuzidisha, na ambao wengine hawakuufikia. Mjengo ulikuwa imara na wa kweli, hata hapakuwa na mahitaji ya kugeuzwa na wale waliokuja baada yake.TSHM 36.3

  Kazi kubwa ambayo Wycliffe alianzisha ni kufungua mataifa yaliyofungwa na Roma wakati mrefu iliyokuwa na msingi wake katika Biblia. Hapa ndipo chemchemi ya kijito cha mibaraka kilicho tiririka tokea zamani za miaka tangu karne ya kumi na ine. Aliye fundishwa kuona Roma kama utawala usiekuwa na kosa na kukubali heshima isiyokuwa na swali kwa heshima ya mafundisho na desturi za miaka elfu, Wycliffe akageukia mbali na mambo haya yote ili kusikiliza Neno Takatifu la Mungu. Badala ya kanisa inayosema kwa njia ya Papa, alitangaza mamlaka moja tu ya kweli kuwa sauti ya Mungu inayosema kwa njia ya Neno lake. Na alifundisha kwamba Roho Mtakatifu ndiyo mtafsiri wake pekee.TSHM 36.4

  Wycliffe alikuwa mmoja wapo wa Watengenezaji wakubwa. Alikuwa sawa sawa na wachache waliokuja nyuma yake. Usafi wa maisha, juhudi imara katika kujifunza na kazi, uaminifu daima, na upendo kama ule wa Kristo, vilikuwa tabia ya mtangulizi wa watengenezaji wa kwanza.TSHM 36.5

  Biblia ndiyo iliyomfanya vile alivyokuwa. Majifunzo ya Biblia itakuza kile fikara, mawazo ya ndani, na mvuto wa roho ambao kujifunza kwengine hakuwezi. Hutoa msimamo wa kusudi, uhodari na ushujaa. Juhudi, kujifunza kwa heshima kwa Maandiko hutolea ulimwengu watu wa akili nyingi, pia na wa kanuni bora, kuliko hekima ya kibinadamu.TSHM 37.1

  Wafuasi wa Wycliffe, walijulikana kama “Wycliffites” na “Lollards”, wakatawanyika kwa inchi zingine, wakichukua injili. Sasa kwa sababu mwongozi wao aliondolewa, wahubiri wakatumika na juhudi nyingi kuliko mbele. Matukano makubwa wakaja kusikiliza. Wengine wa cheo kikubwa, na hata bibi wa mfalme, walikuwa miongoni mwa waliogeuka. Katika pahali pengi mifano ya sanamu ya dini ya Roma iliondolewa kutoka ndani ya makanisa.TSHM 37.2

  Lakini mateso makali yakazukia kwa wale waliosubutu kukubali Biblia kama kiongozi chao. Kwa mara ya kwanza katika historia ya inchi ya Uingereza amri ya kifocha wafia upinzani wa kufungia watu wa dini kiliamriwa juu ya wanafunzi wa injili. Kifo ao mateso ya wafia dini ikafuatana na kufuatana. Wakawindwa kama adui za kanisa na wasaliti wa nchi, wateteaji wa ukweli wakaendelea kuhubiri katika mahali pa siri, kutafuta kimbilio katika nyumba za maskini, na mara nyingi kujificha mbali ndani ya matundu na mapango.TSHM 37.3

  Ukimia, uvumilivu, wa kutokubali uchafu wa imani ya dini ukaendelea kuenezwa kwa karne nyingi. Wakristo wa wakati ule wa mwanzo walijifunza kupenda Neno la Mungu na kwa uvumilivu waliteswa kwa ajili yake. Wengi wakatoa mali yao ya kidunia kwa ajili ya Kristo. Wale walioruhusiwa kukaa katika makao yao kwa furaha wakakaribisha ndugu zao waliofukuzwa, na wakati wao pia walipofukuzwa, wakakubali kwa furaha ya waliotupwa. Hesabu haikuwa ndogo ya waliojitoa bila woga ushuhuda kwa ukweli katika gereza za hatari na katikati ya mateso na miako ya moto wakifurahi kwamba walihesabiwa kwamba walistahili kujua “ushirika wa mateso yake”. Machukio ya watu wa Papa hayakuweza kutoshelewa wakati mwili wa Wycliffe ulidumu katika kaburi. Zaidi ya miaka makumi ine baada ya kufa kwake, mifupa yake ikafufuliwa na ikaunguzwa mbele ya watu, na majibu yake ikatupwa kwa kijito kando kando. “Kijito hiki”, asema mwandishi mzee,majifu yake “yakachukuliwa katika Avon, Avon katika Severn, Severn katika bahari nyembamba, bahari nyembamba katika bahari kubwa. Na kwa hivyo majifu ya Wycliffe inakuwa mfano wa mafundisho yake, ambayo sasa yametawanyika ulimwenguni mwote.”TSHM 37.4

  Katika mafundisho ya Wycliffe, Jean Huss wa Bohemia aliongozwa kuachana na makosa mengi ya kanisa la Roma. Kutoka Bohemia kazi ikapanuka kwa inchi zingine. Mkono wa Mungu ulikuwa ukitayarisha njia kwa ajili ya Matengenezo makubwa.TSHM 38.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents