Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ukaidi wa Dini Unaonekana

  Tangu wakati huu, ushupavu wa dini ukaanza kuonekana. Wengine wakaonyesha juhudi za ukaidi. Mawazo yao ya ukaidi yakakutana na kutokuwa na huruma kwa jamii kubwa ya Waadventiste, ndipo wakaleta laumu juu ya kazi ya ukweli.TSHM 189.3

  Shetani alikuwa akipoteza watu wake, na kwa kuleta laumu kwa kazi ya Mungu, akatafuta kudanganya wengine waliokubali imani na kuwaendesha kwa nguvu kwa kupita kipimo. Ndipo wajumbe wake wakawa tayari wakivisia kupata kosa lo lote, kila kitu kisichokuwa kitendo cha kukubaliwa, na kulishikilia katika hali ya kupita kipimo ili kufanya Waadventiste wachukiwe. Kama angeweza kuleta watu wengi wa kutangaza imani ya kuja kwa mara ya pili, wakati uwezo wake ungeendelea kutawala mioyo yao, angepata faida Kubwa.TSHM 189.4

  Shetani ni “mushitaki wa ndugu zetu.” Ufunuo 12:10. Roho yake inaongoza watu kutazama makosa ya watu wa Bwana na kuwashikilia akiwatangaza, lakini matendo yao mema yanapita bila kutajwa.TSHM 190.1

  Katika historia yote ya kanisa hakuna matengenezo yaliyofanywa bila kukutana na vizuizi vikubwa. Po pote ambapo Paulo alisimamisha kanisa wengine waliojidai kupokeo imani wakaingiza ujushi. Luther pia alivumilia kwa watu washupavu waliojidai kwamba Mungu alinena kwa njia yao, walioweka mawazo yao wenyewe juu ya Maandiko. Wengi walidanganywa kwa njia ya waalimu wapya na wakaungana na Shetani kwa kuondoa kwa nguvu mambo ambayo Mungu aliongoza Luther kujenga. Wesleys alikutana na werevu wa Shetani katika kusukuma katika ushupavu watu wasiyokuwa imara na wasiotakaswa.TSHM 190.2

  William Miller hakuwa na huruma kwa ushupavu. “Ibilisi,” akasema Miller, “anakuwa na nguvu nyingi kwa mioyo ya wengine kwa siku ya leo.” “Mara nyingi, uso wa kungaa na upendo, shavu, lililolowana, maneno ya kukatwa na machozi, vimenipa ushahidi wa utawa wa moyo kuliko makelele yote katika ukristo.”TSHM 190.3

  Katika matengenezo adui zake wakashitakiwa maovu ya ushupavu juu ya wale waliokuwa wakiomba sana kukataa ushupavu. Mwendo wa namna ileile ulikuwa ukifuatwa na wapinzani wa kazi ya kiadventiste. Hawakutoshelewa na kuzidisha makosa ya ushupavu, wakaeneza taarifa ambazo hazikuwa hata na uhusiano kidogo wa kweli. Amani yao ilikuwa ikisumbuliwa na kutangazwa kwa Kristo kuwa mlangoni. Waliogopa ingeweza kuwa kweli, huku wakatumaini kwamba haikuwako. Hii ilikuwa siri ya vita yao kwa kupinga Waadventiste.TSHM 190.4

  Mahubiri ya ujumbe wa malaika wa kwanza yalielekea mara kukomesha ushupavu. Wale walioshirikiana kwa kazi hizi kubwa walikuwa katika umoja; mioyo yao ilijazwa na upendo wa mtu kwa mwenzake na kwa ajili ya Yesu, ambaye walimtazamia kumwona upesi. Imani moja, tumaini la baraka moja, wakahakikisha ngabo juu ya mashambulio ya Shetani.TSHM 190.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents