Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Imani Inaimarishwa

  Roho ya Mungu ilikuwa ingali inakaa kwa wale ambao hawakukataa nuru kwa wepesi waliopokea na kulaumu ujumbe wa kurudi kwa Yesu “Basi, msitupe mbali matumaini yenu, kwa maana yana zawadi kubwa. Kwa sababu munahitaji uvumilivu, ili mukikwisha kufanya mapenzi ya Mungu, mupate ile ahadi. Kwa kuwa bado kidogo sana, Yeye anayekuja atakuja, wala hatakawia. Lakini mwenye haki ataishi kwa imani: Naye kama akirudi nyuma, roho yangu haina furaha naye. Lakini sisi si watu wa kurudi nyuma kwa kupotea, lakini sisi ni pamoja nao walio na imani ya kuokoa roho zetu.” Waebrania 10:35-39.TSHM 194.3

  Onyo la upole hili linaambiwa kwa kanisa katika siku za mwisho. Linaonyeshwa kwa wazi kwamba Bwana angetokea kwa kukawia. Watu hapa walioambiwa walifanya mapenzi ya Mungu katika kufuata uongozi wa Roho yake na Neno lake; lakini hawakuweza kufahamu kusudi lake katika maisha yao. Walijaribiwa kwa mashaka kwamba Mungu alikuwa akiwaongoza kwa kweli. Kwa wakati huu maneno yalikuwa ya kufaa: “Sasa mwenye haki ataishi kwa imani.” Wakainama kwa matumaini ya kukata tamaa, wangaliweza kusimama tu kwa imani katika Mungu na kwa Neno lake. Kwa kukana imani yao na kukana uwezo wa Roho Mtakatifu ambaye alitumikia katika ujumbe ingekuwa kurudi nyuma kwa uharibifu. Maendeleo yao tu ya salama ilikuwa nuru waliokwisha kupokea kwa Mungu, kuendelea kuchunguza Maandiko, na kungoja kwa uvumilivu na kukesha kwa kupokea nuru zaidi.TSHM 194.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents